RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

IBADA YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA MWENGE: HAUTAWAONA TENA MAADUI ZAKO

Kama ilivyokawaida, Rumafrica Jumapili hii ya 11/01/2015 iliweza kuhudhuria ibada ya pili. Katika ibada hiyo kulikuwa na upako wa aina yake kutoka kwa Mungu kupitia mctumishi wake kutoka Mwanza Mch Victor Gasper. Mungu aliweza kuachia ujumbe wake kwa kupitia mtumishi wake huyu ambao leo hii unaweza kubadilisha maisha yako kama utausoma na kufanyia kazi. Somo lenyewe lilikuwa kama ifuatavyo:

Mch. Victor Gasper Malamla akifundisha katika ibada ya pili Efatha Mwenge Dar es Salaam

HAUTAWAONA TENA MAADUI ZAKO
Kutoka 14:5-13. Tumepewa mwaka 2015 wa mabadiliko kwa wana wa Mungu, mabadiliko haya ni lazima yatokee na sio ombi.Huu ni mwaka wa udhihirisho kwa Mungu, Mungu anapotembea na wewe ujue kuna nguvu ya Mungu. Mungu tunaye mtumikia ni Mungu mwenye nguvu.

Kwa nini tunawaona maadui zetu mbele yako?

 1. Kukaa mbali maagizo
Unapofanya agizo na aliyetumwa na Mungu, basi ndani ya hilo agizo kuna nguvu za Mungu au Yesu Kristo. Unapokutwa na mabaya uwe mwepesi wa kufikiri na sio kukimbilia maombi. Unapokaa mbali na agizo tunaona adui anajitukuza katika maisha yako (famillia, mipango, ndoa, biashara yako). Adui anakaa malangoni pako kwani anajiona ana uhalali wake

2. Kusahau asili yako wewe ni nani
Usijilinganishe na watu wa dunia maana aliye ndani yako ni (Petro 1:9) mkuu. Sisi ni uzao mteule, ni watu wa pekee, sisi ni uzao wa kifalme, mfalme mara nyingi haombi bali anaamrisha. Sisi tumepewa amri ya kuamrisha na sio kubembeleza. Mungu afanye makubwa katika kazi zako

Efatha Mass choir wakimtumikia Mungu kwa uimbaji mkuu.

3. Hali ya kumzoea Mungu
Unaona mtu amepona kwa kuombea wewe unaona kawaida. Roho ya kuzoelea inatesa Watanzania wengi sana, watu wamewazoea watumishi wa Mungu na kuwachukulia kirahisi

Bwana Emilot ambaye amemwamini Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, na maono ya mke aliye muoa aliyapata hapa Efatha na mke wake kujifungua salama aliamua kuchora picha ya Mtumishi na leo alikuja kumpa zawadi kama shukrani.

4. Watu hawaheshimu watumishi wa Mungu
Kwa kadiri unavyojinyenyekeza na kujifanya mdogo kwa Mungu, ndipo Mungu anachukuwa alichonacho na kukuachia. Ndani ya watumishi wa mungu kuna kitu ambacho unakitaka, unapaswa kuwa na imani ili uweze kupokea kile alichonacho mtumishi wa Mungu


5. Usizoe matakatifu ya Mungu
Umeacha kweli na kutafuta mafumbuzi yako mwenyewe. Unapokuwa ndani ya huduma fulani basi tembea kutokana na makusudio ya huduma hiyo. Unapokuwa karibu na Mungu ndipo maadui (Zaburi 108: 13) zako wanakuwa mbali na wewe. Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, ndani ya Makuu shetani naye hujiinua, maadui wanapoinuka basi Mungu huwakanyaga watesi wako

Nguvu ya mtembeo wa Mungu inatumwa kwako ili iweje?

 1. Kuuwa adui zako
Inakimbiza adui zako na kukaa mbali na wewe

2. Kuachilia utiisho
3. Kuharibu kazi za adui zako
4. Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika (Isaya 30:29-30
5. Kumshinda shetani

Leo tunaondoka na furaha ya moyo. Inabidi kufika kipindi cha kuacha kulia na kuomboleza na badalayake kumcheka shetani (Zaburi 2:4) . Mataifa wamejipanga ili wakuangamize, lakini kitendo cha kucheka kwa Mungu adui yako anaangamizwa. Kumshinda shetani kwa mkogo ni kucheka na kufurahi (Wakolosai 2: 14-15) . Baada ya Kristo kuja duniani shetani akataka kumpeleka msalabani .

Adui zako wanaweza kukuona unaenda Kanisani na wao wanasema unaenda kama kawaida kuwa wameshakumaliza, lakini leo nataka kusema wameshindwa.

SHUHUDA
Mama huyu ambaye ameshikilia zawadi ya picha ya Nabii na Mtume Josephate Mwingira ambayo ilichorwa na mume wake ambaye ni mzaliwa wa Uganda na ameoa Mtanzania. Mama huyu aliweza kushuhudia jinsi Mungu alivyomponya kwa kupia picha ya Nabii na Mtume Mwingira. Mama huyu aliteseka sana na uchungu wa kuzaa baada ya kupata maumivu ya uchungu zaidi ya miezi kadhaa. Madaktari walieza kumsaidia lakini ilishindikana na kila dakatari aliyempima alimuona huyo mwanamke kuwa hana ujauzito.

Mume wake kwa imani aliweza kwenda kwenye mitandao na kutafuta picha ya Mtume na Nabii Mwingira na baada ya kupata aliweza kwenda nayo kwa mke wake. Mke huyu baada ya kupata ile picha aliweza kupata uchungu tena na kuzaa.



Comments