RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

JINSI TAMASHA LA JANE MISSO MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA LILIVYOFANA SIKU YA JUMAPILI 11.01.2015 KATIKA KANISA LA KKKT MABIBO EXTERNAL UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

Nwandishi na mpiga picha: Rumafrica

Rumafrica ina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kupata kibali cha kuweza kufika katika tamasha la mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania mtumishi Jane Misso siku ya jana Jumapili 11.01.2015 katika kanisa la K.K.K.T Mabibo External Ubungo jijini Dar es Salaam - Tanzania.

Mtumishi wa Mungu Jane Misso alikuwa akizindua albamu yake ya USIKUMBUKE REMIX Vol.3 na kuweka wakfu kwa Mungu wetu wa mbinguni ili ikafanyika baraka na uponyaji kwa watu wenye mateso mbalimbali.


Tamasha hili lilihudhuriwa na waimbaji mbalimbali na kwaya mbalimbali kama utakavyoona hapo chini. Tunamshukuru Mungu kwa waimbaji ambao walifika mahali hapa na kufanya kazi ya Mungu kwa moyo wao wote na kwa upendo. Tamasha hili kwa kweli lilipendeza sana kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Waimbaji walikuwa wengi sana mpaka wengine wakakosa hata muda wa kuimba. Waimbaji kuanzia mwanzo hadi mwisho walikuwa wako bize na kuselebuka kwa utukufu wa Mungu, hakuna hata mwimbaji aliyeweza kuonyesha kuchoka kucheza na hii ni kutookana na kutambua siri mojawapo kumtukuza Mungu wetu wa mbinguni.


Rumafrica iliweza kushuhudia kuona watu walivyoitikia na kufuarahia waimbaji wao na wengine waliweza kutoa fedha zao kutokana na mafuta ya upako yaliyo ndani ya uimbaji wao. Kutokana na maisha kuwa magumu sana, si rahisi kuona mtu anatoa fedha zake nyingi kwa mtu wakati maisha ni magumu, ukiona kuna mtu anafanya hivyo basi utambue mtu huyo amebarikiwa sana na uimbaji wako.


Mgeni rasmi wa tamasha hili alikuwa Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni Mh. Fenella Mkangaa lakini hakuweza kufika kutokana na muingiliano wa ratiba na hivyo ikamlazimu kumtuma Naibu wake kumuwakilisha. Tunamshukuru sana mwenyezi Mungu kwa kumuwezesha huyu mgeni rasmi kuwakilisha mchango wake mkubwa sana ikiwa ni pamoja na kuchangia mabati 100 kwaajili ya ujenzi wa shule ya watoto wadogo. Shule hii ya Nursery ni maono ya mtumishi wa Mungu ambayo amepewa na mwenyezi Mungu baada ya kuona kuna baadhi ya wananchi wanahangaika kuwapeleka watoto wadogo kupata elimu katika shule zilizopo mbali na mahali wanapoishi.


Waimbaji wa nyimbo za Injili wakiongozwa na mtumishi wa Mungu Bahati Bukuku waliweza kuwashukuru watumishi wa Mungu yaani wachungaji wa kanisa hili ambao waliweza kuwakaribisha na kumruhusu Jane Misso kufanya tamasha lake, na pia waliwashuru watu wote waliofika katika tamasha hilo na jinsi walivyojitoa kutoa michango yao kwaajili ya ujenzi wa shule ya watoto.

Mtumshi wa Mungu Jane Misso alimshukuru sana Mchungaji wa kanisa hili, mgeni rasmi na muwakilishi wake, wapenzi na wadau wa nyimbo za Injili, waimbaji waliofika katika tamasha hilo, waandishi wa habari na kila mtu kwa nafasi yake kwa kufika na kumuunga mkono. Jane Misso aliwaombea Mungu kuwabariki watu wote walioweza kufika na wengine walioshindwa kufika kutokana na sababu zisizozuilika.


Sasa ngoja matukio
 Tangazo la tamasha la Jane Misso lililotengenezwa na Rumafrica +255 715 851 523
 Kanisa la KKKT Mabibo Externa Ubungo katika muonekano wake wa nje


Sarah Mvungi


Eneo la waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania

Apostle John Komanya akiimba

Apostle John Komanya akiwa na waimbaji wenzake wa JOY Band


Apostle John Komanya

Beatrice Mwaipaja

Katikati ni Beatrice Mwaipaja

Ammy Mwakitalu

Edson Mwasabwite
 Edson Mwasabwite
 Edson Mwasabwite (katikati)


MC Christina Matai

Muwakilishi wa mgeni Rasmi akiingia kanisa kwa uzinduzi
 Kulia ni muwakilishi wa mgeni rasmi

JANE MISSO AKIINGIA MADHABAHUNI TAYARI KWA KUKABIDHI ALBAMU YAKE KWA MUNGU KWA KUIZINDUA

 Jane Misso (wa nne kutoka kulia) akiwa mlangoni tayari kuelekea madhabahuni. Kutoka kulia ni Edson Mwasabwite, Christopher Muhangila, Bahati Bukuku na Jane Misso.

 Jane Misso (kushoto) na Bahati Bukuku (kulia)
 Bahati Bukuku akisalimiana na muwakilishi wa mgeni rasmi
 Mstari wa mbele kutoka kulia ni Leah, Tumaini Njole, Bahati Bukuku na Jane Misso
 Atosha Kissava (wa pili kutoka kulia-mstari wa mbele)

 Leah (kushoto) na Atosha Kissava (kulia)



KIPINDI CHA KUSOMA RISALA
 Bahati Bukuku akisoma Risala kwa muwakilishi wa mgeni rasmi
 Bahati Bukuku





 Tumaini Njole akimkabidhi ua la upendo kwa muwakilishi wa mgeni rasmi
 Muwakilishi wa mgeni rasmi akiwakilisha mchango aliotumwana mgeni rasmi Mh. Fenella Mkangaa ambaye ni Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni
 Mc Joshua Makondeko (kushoto)

KIPINDI CHA KUIOMBEA ALBAMU YA USIKUMBUKE REMIX YA JANE MISSO
 Lilian akiwa ameshikilia albamu ya USIKUMBUKE REMIX wakati watumishi na mgeni rasmi wakiiombea















KIPINDI CHA MUWAKILISHI WA MGENI RASMI KUONDOKA BAADA YA KUMALIZA KUZINDUA ALBAMU YA JANE MISSO
 Apostle John Komanya (kushoto)


KIPINDI CHA KUMUUNGA MKONO JANE MISSO KWA KUTOA MICHANGO NA ZAWADI MBALIMBALI
 Rosen Joel akiwa tayari kuandika majina ya watoaji wa michango

 Leah (aliyesimama kulia) akijiandaa kwa kuandika majina ya watu wanaomuunga mkono Jane Misso


 Mtoto akiombea ili aweze kuwa mwimbaji wa kimataifa miaka ijayo

 Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji) kushoto akitoa ahadi yake ya kumuunga mkono Jane Misso
 Masanja Mkandamizaji akiahidi kumchangia Jane Misso


 Bahati Bukuku akiwa bize sana kuuza albamu ya Jane Misso











 Mtangagzaji wa Channel Ten na Praise Power Bony Magupa (BM) (alieshika mic)
 Atosha Kissava akiimba
 Madam Ruti akiimba

 Tumaini Njole katikati akiimba
 Manesa Sanga akiimba

KIPINDI CHA KUFUNGA TAMASHA
Bahati Bukuku akiwa na waimbaji wenzake wakifunga tamasha kwa kuwashukuru watu wote waliofika kumuunga mkono Jane Misso







Comments