RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MTUMISHI HUYU KWELI ATATUFIKISHA MBINGUNI WAKATI YEYE NI MZINZI AMESWA NA MKE WA MTU

Mbona nyinyi watumishi mnatupeleka jehanamu??? . Mambo wanayotufundisha kanisani tofauti sana na maisha wanayoishi, wamekuwa wongo hata madhabahuni. Watumishi mnatudanya na kutufanyia usanii waumini wenu. Nakemea  tabia zenu mbaya za kutudharirisha waumini wanu. Mungu na awapige na kuwaanika ili kila mtu ajue upuuzi wenu mnaofanya.

Achane kabisa kumchezea Mungu wetu aliye mtakatifu, ninasema hili kwa uchungu sana. Mnawachezea wake za watu kwa kuwadanganya na pesa tunazotoa waumini wenu.

Na wewe mwanamke unayejua kabisa huyu unayeenda naye kuzini si mume wako na ni mtumishi wa Mungu, huna haya kabisa wewe mwanamke. Na kama hujabambwa basi ujue siku yako inakuja na utawekwa kweupe kabisan. Hebu sansa soma chanzo cha fumanizi hiii.

Stori: Waandishi Wetu/Risasi Mchanganyiko
Ohoo, ama kweli dunia imekwisha! Mtumishi wa Mungu (Muinjilisti) ambaye kipindi chake cha dini kinarushwa katika kituo kimoja maarufu cha televisheni Bongo (Jina tunalihifadhi) aliyefahamika kwa jina la Fredrick Kishindo ‘Badoo’ hivi karibuni alipata aibu ya kufungulia mwaka 2015 baada ya kunaswa na mke wa mtu chumbani, Risasi lina mkanda nzima.


Mtumishi Fredrick Kishindo ‘Badoo’ akijistili kwa kanga baada ya fumanizi hilo.

Ilikuwaje?
Awali chanzo cha habari kilichoomba hifadhi ya jina lake kilieleza kuwa, Januari 11, mwaka huu Muinjilisti huyo anayesifika kwa kuhubiri watu waache dhambi alionekana akinyata kuingia kwenye nyumba ya mke wa mtu huyo iliyopo Sinza jijini Dar huku kukiwa na taarifa kuwa, mume wa mwanamke huyo alikuwa safarini.

Wifi mtu atonywa
Ikaelezwa kuwa, kufuatia mazingira hayo wifi wa mwanamke huyo alitonywa juu ya taarifa za Badoo kuingia kwenye nyumba ya kaka yake, maelezo yaliyomshitua hivyo kulazimika kuelekea eneo la tukio.
Baada ya wifi mtu huyo kufika nyumbani kwa kaka yake na kuhakikishiwa kuwa Badoo yuko ndani, aliuliza namna ya kuwapata makamanda wa Operesheni Fichua Maovu ya Global Publishers ‘OFM’ ambapo mmoja wa majirani alimpatia namba ya simu, akawapigia.

...Akivaa shati huku kitendea kazi chake(Biblia) kikiwa nyuma yake.

Polisi washirikishwa
Katika kuhakikisha usalama katika eneo hilo, wifi huyo pia aliwasimamisha polisi waliokuwa doria na kuwatonya juu ya uzinzi unaofanyika nyumbani kwa kaka yake na kwa kuwa kazi ya askari ni kulinda raia na mali zao, walitoa ushirikiano.

OFM watinga eneo la tukio
Baada ya makamanda wa OFM kupigiwa simu na kunyetishiwa juu ya uwepo wa Muinjilisti huyo chumbani na mke wa mtu, kwa kutumia pikipiki zao ziendazo kasi walianza safari na baada ya dakika chache walikuwa wamefika kwenye nyumba hiyo na kuwakuta polisi.

Muinjilisti, mke wa mtu live
Polisi wakiwa na OFM waliongozwa na wifi mtu huyo hadi kwenye chumba ambacho madhambi yalikuwa yakitendeka, walipoingia walikuta mke wa mtu na mtumishi huyo wa Mungu wakiwa kama walivyozaliwa.

Aibu iliyoje!
Baada ya kuona ‘picha imeungua’, mtumishi huyo alisikika akisema kuwa amepata aibu ambayo hakuitarajia huku akiomba asipigwe picha wala kufanyiwa kitendo kibaya bali apewe nafasi ya kujitetea.
Aidha mke wa mtu aliyenaswa akimsaliti mumewe alionekana kutahayari na aliishiwa nguvu zaidi alipomuona wifi yake aliyekuwa amefura ile mbaya.

Mchungaji huyo akijitetea baada ya fumanizi hilo.

Utetezi wa mtumishi wa Mungu
Kufuatia kunaswa huko, Badoo alijitetea kwa kujichanganya, awali alisema aliitwa na mwanamke huyo kwa ajili ya kuongea mambo ya biashara na kwamba eti walivua nguo kutokana na hali ya joto iliyokwemo chumbani humo.

Kana kwamba alihisi kajichanganya, Muinjilisti huyo aligeuza utetezi na kusema aliingia majaribuni baada ya kushawishiwa na ibilisi kisha mwanamke huyo hakumwambia kuwa ana mume.

Bofya hapa usikie utetezi wake
“Jamani naomba mnisamehe, si kosa langu bali ibilisi ndiye aliyenishawishi na huyu mwanamke hakuniambia kama ana mume. Hapa aliniita kwa ajili ya biashara flani.
“OFM nawajueni lakini niko chini ya miguu yenu, naomba msiitoe habari hii gazetini kesho n’tawaletea chochote pale ofisini kwenu, si ni pale Bamaga ee, napajua sana pale”.

Mke wa mtu akijifunika kwa aibu.

OFM ni mwiko kupokea rushwa
Licha ya utetezi wake huo, makamanda wa OFM walisimamia weledi wa kazi yao na kumweleza kuwa, rushwa kwao ni mwiko hivyo kama atafika ofisini kwao iwe ni kwa ajili ya maelezo zaidi ya kwa nini amevunja moja ya amri kumi za Mungu.

Mpaka OFM wanaondoka eneo la tukio, mke wa mtu huyo alikuwa akiendelea kumuomba msamaha wifi yake huku Muinjilisti naye akijaribu kutuliza mambo yasifike mbali akidai kuwa, mke wake, ndugu na marafiki wakijua ataaibika.

Ni fundisho
Gazeti la Risasi limefikia hatua ya kuiandika habari hii ili iwe fundisho kwa watu wengine ambao wamekuwa na tabia ya kuvuruga ndoa za watu ikiwa ni pamoja na kufanya mambo mengine ambayo ni kinyume na maadili.

Comments