RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

EFATHA MWENGE: MLANGO UMEFUNGULIWA MBELE YAKO FANYA NGUVU KUINGIA

Rumafrica Jumapili hii ilibahatika kufika katika kanisa la Efatha Mwenge lililoko jiji Dar es Salaam kwa Mtume na Nabii Josephate Mwingira na kujifunza mambo mengi sana. Kanisa hili lina ibada tatu, Rumafrica ilibahatika kuingia ibada ya pili inayoanaza saa 4 asubuhi mpaka saa 7 mchana. Somo letu lilikuwa kama ifuatavyo likifundishwa na mchunagji kiongozi wa kanisa la Efatha Mwenge (jina halikupatikana)



MLANGO UMEFUNGULIWA MBELE YAKO FANYA NGUVU KUINGIA
Neno la Mungu lina kuja kwetu ili kubadilisha tabia zetu
MAMBO YANAYOHUSU SISI
Tumekua sababu kubwa sisi wenyewe kutofungua mlango wetu.Yakobo4:1-12. Mlango wetu umefunguliwa lakini wapo watu wapingao. Ili  tuweze kupita mlango huo lazima tuwe na Mungu na kutimiza sheria zake .

Picha ya ibada zilizopita

Vita ndivyo vyanzo vinavyo sababisha sisi kutokuingia katika ule mlango. Vita vipo ndani yetu  na mtu wa nje anachochea hivyo vita vilivyo ndani yetu. Lengo la Mungu ni kufungua mlango wake kwetu ili sisi tuwe na utukufu wa Mungu .

Moja ya vita ni tamaa zetu wenyewe ,tunapaswa kuomba sawasawa na mapenzi yetu ,tukiomba kwa tamaa zetu hatupati yale ya Mungu ambayo ameweka kwa ajili yetu .Kuomba kwa mapenzi ya Mungu ni kutaka kuwa karibu na huyu Mungu . Maisha yetu yakiwa ovyo tunamtukana Mungu wetu kwani tunawaonyesha watu kuwa Mungu hawezi. Kuwa rafiki wa dunia nikuwa adui waMungu.

(Picha ya ibada zilizopita)
Tamaa zetu zina zuia maombi yetu kupokelewa na Mungu .Unatakiwa kutafakari jinsi unavyoomba, usiombe ili mtu aone unavyoomba. Utamani kuona majirani  zako wanatamani huo wokovu wako, wewe ni barua kwa mataifa. Roho ana kutamani kukuona una omba sawasawa na mapenzi ya Mungu. Unavyo fanya mambo yasiyompendeza Mungu ,una chelewesha muujiza wako.

Unapoletewa mabaya una takiwa kunyamaza na kuona ni mageni kwako.Yesu alipo tukanwa alinyamaza kimya kwasababu aliona mageni kwake. Unavyo jinyenyekeza Mungu ana kupandisha. Kujinyenyekeza ni kufanya jambo kama hulijui hata kama una lijua.

Unavyo jifanya hujui ukiomba, Mungu ana kufungulia na vile ambavyo ulikua hujui. Tunatakiwa kumtii Mungu kwasababu nguvu iko katika kumtii Mungu  na haipo kwenye maombi tu .Uki mtii Mungu shetani ana kukimbia,shetani hatukimbii etii kwa sababu tupo kanisani bali anakimbia kwa kumtii Mungu
Ukikosea sheria ya Bwana shetani ana kua mlangoni hata kama una omba sana.Sheria ya Mungu ni kumtii Yfsu na kusahau ya nyuma na kusonga mbele.

Unapo kuwa kanisani waza yaliyo ya Mungu kwani huyo ni Baba yako daima. Shetani anatukata padogo na kututesa kwasababu hatufati sheria ya Mungu. Unatakiwa kuwana nia ya kristo na ukifanya hivyo, yaliyokufa yanafufuka .Ili nia iwepo lazima umwambie Kristo akusaidie katika masongamano yanayo kukabili muda huo .

Roho wa kristo yupo ndani yetu na anataka kufungua siri zilizo ndani yetu.Unatakiwa kubadilisha nia yako sasa na achana kuwa na mazoea.
Mungu akitaka kukuondolea kiburi ana kuletea watu wa kukuudhi. Akiona wewe ni mchoyo ana kuletea wageni wengi.
Siku ya  kufanikiwa furahi na siku ya mabaya fikiri . Mungu anasema nimpendae na mkemea na kumrudi yaani kumchapa . Unapokosea muombe Mungu akusamehe na kukurehemu.
Ukiwa unamtaja mara nyingi shetani inaonesha una mheshimu. Unapo muogopa shetani maana yake una mheshimu, lakini unapo mpuuza anakukimbia . Unapomtaja shetani mara nyingi maana yake una mwita akusogelee na kukusikiliza.

Furaha yako igeuze kuwa hamu yakutaka kujua Mungu ana waza nini juu yako. Ni mbaya sana kuzogoana kwa wapendwa, wengine wamepata laana kwasababu ya kuwasema wenzake au walokole wenzake. Tume amriwa na Mungu tupendane kama mwenzako huja mwelewa nyamaza,usipofanya hivyo  utajiletea laana hadi kwenye kizazi chako. Kama umeamua kuokoka acha kumsema vibaya aliye okoka mwenzako, maana ukifanya hivyo utajiletea hukumu mbaya sana.Kunyamaza kwa anaye semwa ni fimbo kwani hujui ni nani alie mnyamazisha. Unatakiwa kumuombea. Unavyo sema hivyo ujue una msema Kristo kwani Yesu yupo ndani yako na huyo mpendwa mwenzako naye ana Yesu.

Unavyomsema vibaya mpendwa mwenzako anakosa hata kuwaombea watu wa Mungu, tuache fujo ndani ya nyumba ya Mungu. Kama mtu amekosea kaa nae chini na ongea nae. Huyo anaemsema vibaya ni wathamani sana kwan Yesu na alikufa msalabani kwa ajili ya huyo unayemsema vibaya.

MUNGU AWABARIKI



IBADA YA TATU

Katika ibada hii walifundishwa somo lifuatalo


TANGULIZA MAMBO MUHIMU KWANZA
Jambo moja muhimu wewe unatakiwa uwe wa muhimu ufanye mambo ya muhimu, hakuna mtu anayefanya mambo ya ovyo ovyo alafu akawa mtu muhimu, fanya mambo ya muhimu ili uwe mtu muhimu. Unaweza ukaona mke wako, gari, kazi, nyumba na watoto ni wa muhimu kumbe sivyo kuna jambo ambalo unatakiwa kulifanya muhimu ndipo vitu vyote vitaonekana muhimu mfanye Mungu wa muhimu kwanza ndivyo vitu vyote kwako vitaonekana vya muhimu. Utafuteni kwanza ufalme wake na vingine vyote mtazidishiwa.


Akihubiri

GLORY AMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA NDOA KATIKA FAMILIA AMBAYO WALIKUWA HAWAOLEWI NA KUBARIKIWA KATIKA BIASHARA YAKE YA MGAHAWA.

Glory Samweli natokea Eneo la Sayuni napenda kumshukuru Mungu kwa ajili ya Baba Josephat pamoja na Maaskofu wangu wote, napenda kumshukuru Mungu amenipa Ndoa katika familia yetu tulikuwa hatuolewi ila kwa sasa ni mimi ambaye ni wa kwanza kuolewa na kuwa ndoa katika familia yetu. Nilijifunza, Baba Mtume na Nabii alisema JIFUNZE kupata maisha ya Ushuhuda, sasa nimeolewa na Ndoa yangu imefanyika mwaka jana tarehe 23/8/2014.

Ilikuwa sikumoja Baba alituambia tucheze ngoma za asili nilikuwa nina maisha magumu lakini nilikuwa nacheza huku nikimwambia Mungu nataka nikuone, na kweli Mungu aliniridhia Baba alinipa shilingi 10,000 nikaanzishe biashara, ila nilivyofika nyumbani nikamwambia Roho Mtakatifu hii hela haitoshi nataka unipe nyingi zaidi ya hii. nikaja kutoa fungu la kumi na sadaka. Siku ya pili ilipofika akaja mtu akasema nataka tufanye biashara, akanipa hela akaniambia chukua hii hela utanirudishia kidogo kidogo. Namshukuru Mungu sasa nina cafe yangu (mgahawa) na unajulikana sana ipo maeneo ya Masaki, namshukuru Mungu sasa nina jina kubwa.



LUCY AMSHUKURU MUNGU BINTI YAKE KUJIFUNGUA SALAMA
Naitwa Lucy Mtege wa Ubungo Maziwa, namshukuru Mungu kwa binti yangu kujifungu salama , jumaplili nilikuja na binti yangu alikuwa anasumbuliwa na pepo la ngono baada ya maombi binti yangu alitoka kwenye kiti akakaa chini akawa anajisikia vibaya na wahudumu walikuja kumchukua wakambeba na walimtoa nje na kumwingiza katika chumba kimoja na ndani ya kile chumba kulikuwepo na madaktari walimwombea na kupona mguu wake aliokuwa analalamika mama mguu unauma, lakini baada ya muda kuombewa maombi akawa mzima, na hakusikia tena yale maumivu ya mguu, na baada yakuachilia mguu mwanangu akaanza kusikia uchungu na kusaidiwa na madaktari akajifungua salama hapahapa kanisani mtoto wa kike anaitwa Eliakunda .





Efatha mass choir wakimsifu na kumwabudu Mungu Ibadani, nifuraha na amani kumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. Karibu uungane nasi kila Jumapili

Comments