RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA EFATHA MWENGE DAR ES SALAAM: MLANGO MKUBWA WA KUKUFAA UMEFUNGULIWA FANYA NGUVU KUINGIA

Ibada ya Jumapili ilikuwa ni ya namna yake katika kanisa la Efatha Mwenge lililopo jijini Dar es Salaam Tanzania. Rumafrica ilibahatika kufika katika kanisa hili na kujifunza mengi sana, na baadhi ya mafundisho hayo ni haya hapa chini, karibuni tushiriki Neno la Mungu

Vita vyatoka wapi? Vita vipo ndani ya mtu, vinavyoanza kupigana vita ni ufahamu wa mtu na akili zake, jirani anaweza kukwaza asilimia 20, na asilimia 80 ni za kwako. Kama hujaponyeka kiroho ni rahisi kukwazika, kama mtu anakwambia wewe mpumbavu usilie kwa sababu wewe sio mpumbavu kama watu wanavyosema. Leo tutaendelea na somo la Jumapili iliyopita linalosema, “Mlango Mkubwa wa Kufaa Umefunguliwa Fanya Nguvu Kuingia”

Kulia ni Mchungaji alihubiri Jumapili hii

Wakorintho 1:9
Kwa maana umefunguliwa mlango mkubwa wakufaa na wapo wengi wakupingao, lazima tujiulize ni akina nani wakupingao? Ukisema unampinga shetani lazima ujue huyo shetani yuko wapi? Kwa hiyo unavyotaka kumpinga shetani/ adui lazima umtafute yuko pande gani ndipo umpige.

Waefeso 5:1
Unapokwaza ni bora kushukuru na sio kuendelea kukwaruzana , tunatakiwa kumfuata Mungu kama mtoto aliyependwa, na tunatakiwa kuenenda katika UPENDO. Upendo huvumilia, hauhesabu makosa, haujivuni.

Yesu alipoudhiwa na wanadamu yeye alisema nawapenda wote, tunatakiwa kuelewa injili inasema nini juu ya upendo. Tunatakiwa kuwa kama watoto walivyo na upendo, wakati mtu amekukwaza wewe nenda kwa upendo kama Kristo alivyotupenda na kujitoa sadaka kuwa harufu ya manukato. Unapokuwa na upendo unakuwa harufu na manukato.

Unapoambiwa toa dhabihu ni wakati wa kuacha yale ya kale, Bwana anasema usitajwe uasherati wala uchafu wowote kwa watakatifu. Watu wengi wanaposikia ovu wanazidi kusambaza habari za uovu hilo ni jambo baya.

Mlango unaweza kuzuiliwa kutokana na tabia yako , kwa mfano ubishi, hata ukiambiwa jambo la kweli wewe unabisha, amua kutumia kinywa chako vizuri na ukifanya hivyo adui atashindwa kuja kwako. Jambo lolote linavyokuja kwa mtu linasababu.

Yohana 15:7
Maneno ya Mungu yakikaa ndani yako na yeye akikaa ndani yako, omba lolote naye atakupa/ utatendewa. neno la Mungu linaweza kupita katika ule mlango, unatakiwa kujiuliza wewe unawaza nini na kinywa chako kinanena nini? Nena katika kinywa chako maneno makubwa ili yaweze kutokea katika maisha yako, maneno ya kipuuzi yasiwe ndani mwenu. Heri kuwa mtakatifu, mtu akikutukana wewe sema asante, hautakiwi kunena mambo ya kushindwa bali nena maneno ya kushinda kwani yatakusaidia katika mafanikio yako. Amua kuacha mambo ya kijinga katika kinywa chako ili uweze kupokea Baraka zako. unatakiwa kubadilisha mawazo ya kusema maisha ni magumu bali sema hakuna hali ngumu, ukifanya hivyo utaona mambo yakibadilika.

Ondoa aibu ndani yako, unapokuwa na shida mshirikishe mwenzako utaona mambo yakibadilika, mtafute rafiki mwenye nia ya kukusaidia, ili aweze kukusaidia hata kwa mawazo.

Kuna watu wanaujuzi Fulani na wanakarama Fulani lakini wanashindwa kuwashirikisha wenzao. Ukikaa kimya na ujuzi wako au karama yako utambue haitakuja kukuwa kamwe, utabaki na level hiyo hiyo ya ujuzi.

Kupokea Baraka kwa vinywa vyetu vitatupa ufinyu sana wa mambo kufanyika, unatakiwa kufanya kazi baada ya kupokea hiyo Baraka yako. Unatakiwa kujibidisha kwa kila jambo unalofanya ili uweze kufikia malengo yako, acha kuongea ya giza bali ongea ya nuruni.

SHUHUDA MBALIMBALI

ESTER DAVID MSIMBI ASHUHUDIA KUPATA DIVISION ONE KIDATO CHA NNE
Nilikuwa na Kibao cha Marufuku kwamba Siwezi kufaulu, lakini baada ya Kuomba na Kuvunja Kibao hicho, Nimefaulu na Nimepata DIVISION ONE.

Ester David Msimbi: Napenda kumshukuru MUNGU, katika kusoma kwangu nimekuwa nikifanya vizuri lakini nilikuwa sishiki Nafasi ya Kwanza, nilikuwa namaliza Kisutu Sekondari, wakati huo nilikuwa na mambo yangu mengi ya uongozi, nilikuwa sifanyi vizuri, nilipokuwa nafanya Mitihani nilikuwa sipati zile Division zinazo takiwa.

Lakini baada ya Mafundisho ya Mchungaji wangu Mama Mdadila aliposema kuna “KIBAO cha Marufuku” kimeandikwa mbele yangu kwamba Sitafaulu, akasema “TUKIVUNJE” kile kibao, na baada ya Kuomba na Kuvunja kile kibao MUNGU Aliniona na Kunisaidia, nimepata Division ONE.

Na kuna maneno magumu kutoka kwa baba yangu mzazi alinitamkia, ya kwamba nitafeli nitapata ziro - ziro lakini MUNGU alijiinua kwangu na kunipa Kibali kwa Mwaka huu wa (Mtembeo Wa MUNGU Kwa Wale Alio Waridhia) nimepata Divison One. Lakini hii yote ni kwa sababu nilikuwa najitahidi sana katika masomo yangu lakini pamoja na hayo kuna kitu kilikuwa kinanizuia kufikia Division one, kila ninapo jitahidi nafasi yangu ilikuwa inachukuliwa na mwingine lakini MUNGU wa Efatha kutokana na maombi ya Mama Mchungaji Mdadila nimefaulu, namshukuru MUNGU sana Amina

ASHUHUDIA KUPATA MTOTO BAADA YA KUKAA MIAKA 5 BILA MTOTO
YESU YU HAI, NI YULE YULE
SHUHUDA: Wana wa MUNGU wakishukuru MUNGU wetu MKUU
kupata Mtoto baada ya Kukaa miaka 5.

Wana wa MUNGU pichani, waliamua kuja mbele ya Wana wa MUNGU, kuja Kumshukuru MUNGU MKUU kwa Matendo Makuu waliyotendewa, walikaa miaka 5 bila kupata Mtoto, walitiwa Nguvu na Mwana Efatha aliyekuwa anakaa nao jirani, aliwaambia "Msikate tamaa, MUNGU wetu ANAWEZA, YESU WETU YU HAI, YESU NI YULE YULE, YU HAI, ATAWAPA ITAJI LENU LA MOYO", Walizidi kuendelea Kuomba Kila siku,..

SIFA NA UTUKUFU NA UKUU ni kwa MUNGU WETU BABA YETU MKUU, AMETENDA, Hakuna JAMBO GUMU KWAKE, YEYE NI MUNGU si Binadamu, ANAWEZA, YU HAI, HAKUNA LINALOMSHINDA, Hata wewe hapo TAZAMIA KICHEKO CHAKO Sasa, POKEAAAAAA....