Jumapili ya 15.03.2015, Rumafrica iliweza kufika katika kanisa la Efatha Mwenge lililoko Dar es Salaama katika ibada ya pili inayoaanza saa 4:00 asubuhi na kumalizika saa 7:00 mchana na kujifunza mengi kwa mchungaji Thadeo Msuya aliyekuwa akihubiri siku hiyo. Tulijifunza juu ya kuuruhusu mwili wako ufanyike dhabihu
Pichani: Mch. Thadeo Msuya aliyesimama katika Ibada ya Neno Ibada ya pili.
KUBALI MWILI WAKO ILI UWE DHABIHU
Tusome Warumi 12:1-2, tunatakiwa kutoa miili yetu kwaajili ya kazi ya Bwana. Kusudi la kanisa la Efatha duniani ni kuaandaa kanisa la mwisho kwaajili ya unyakuo. Kila kiungo kinatakiwa kufanya kazi ya Mungu na miili yetu ifanye dhabihu.
Katika miili yetu kuna vikwazo, lakini unatakiwa kumuomba Roho Mtakatifu akuongoze na kukushindia vikwazo na ufanyike dhabihu. Kumbuka katika kazi unayofanya utaitolea hesabu kwa Mungu.
Mwaka huu Mungu anataka kutembea naye kwani kuna mlango mkubwa sana umefunguliwakwako wewe kuingia kama utafanya yale Mungu akuagizayo. Mwili wako ukiwa dhabihu, utii na utakatifu utakula mema ya Mungu.
Hatupaswi kuwa watu wavivu katika kazi ya Mungu, Tumuombe Mungu atusaidie na atusamehe pale ambapo hatukutumia miili yetu kwa kazi ya Mungu. Ukiwa na dhabihu unaweza kufanya mambo makubwa ya Mungu na ukafanyika baraka.
Unatakiwa kuwa mtu wa maombi, uwaombee wenye uhitaji, fanyika dhabihu kwa kufunga na kuomba. Toa mwili wako kuwa dhabihu ili kutoa maumivu uliyokuwa unateseka nayo, na usipofanya hivyo utatoa hesabu kwa Mungu siku ya mwisho. Ukikubali na kusema kila kitu ulichonacho kuwa dhabihu kitu hicho kitaweza kufanya mambo makubwa kwa jamii inayokuzunguka.
Katika mazingira unayoishi, jirani zako wajue umeokoka kwa kufanya yale ambayo yatasababisha hawa watu kuamini kuwa wewe ni mtu uliyeokoka na sio wa kubahatisha. Watu wengi wanakosa kufanya makubwa kwasababu miili yao haijafanyika dhabihu. Unatakiwa kuithamini nafsi yako uliyopewa na Mungu na kuiheshimu. Mungu akubariki sana
KIPINDI CHA MAOMBEZI KIKIENDELEA
Pichani: Wana wa Mungu wakiwa katika Ibada ya maombi Ibada ya kwanza Efatha mwenge Dar es salaam Tazania
SHUHUDA MBALIMBALI KUTOKA KATIKA KANISA LA EFATHA
ANASATAZIIA ASHUHUDIA JINSI ALIVYOKUWA AKISUMBULIWA NA KUTOKWA NA UTUMBO KATIKA SEHEMU YA HAJA KUBWA AKIJISAIDIA KIPINDI MJAMZITO
Naitwa Anastazia mmasa namshukuru Mungu kwa yale aliyonitendea nikiwa nina hii mimba ya mtoto huyu nilikuwa nikijisaindia haja ndogo na utumbo mrefu ulikuwaa unatoka nikawa na maumivu makali sana na nilpoenda hospitali mnazi mmoja daktari aliniambia niende muhimbili na lipofika nikakuta kuna foleni sana niliamua kurudi mnazi mmoja wakaniambia nikanunue dawa na nilipoanza kutumia zile dawa nikawa napata maumivu sana na zilikuwa zimebakia dawa za siku tatu nikamwambia yesu naomba unihurumie mimi mtumishi wako .
Siku za kujifungua zilipofika mama Chitete akaniambia unamwamini Mungu wa Efatha kuwa anaweza ? nikamwambia Amen na muda wa kujifingua ulipofika niliingia leba ya Efatha na mpaka jioni nikawa sijajifungua nikapelekwa mhimbili baada ya muda mfupi nilijifungua salama nikiwa pale hospitali dada mmoja alikuwa anatakiwa afanyiwe upasuaji lakinialiponiona nimejifungua kwa muda mfupi baada ya kufika hospitalini akasema mimi nataka nijifungu kama huyu dada na kweli ikawa kama alivyosema
ADAM ADAM APONA NA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA MKOA WA IRINGA BAADA YA GARI LAKE KUPINDUKA KATIKA SHIMO AMBALO LILISABABISHA AJABLI MBAYA SANA YA BASI NA KUUWA WATU WENGI
Adam Adam, Namshukuru Mungu nilikuwa naendesha gari aina ya noah nilikuwa naenda Mbeya, nilipofika Iringa lile eneo ambalo gari ya Manjinjah na lori lilipata ajali mimi niliingia kwenye lile shimo lililowaua wenzangu na baada ya hapo gari yangu matairi ya nyuma yalipasuka yote gari likapinduka mara nne lakini sikupata majeraha ya aina yeyote na nilitoka mzima nikiwa na akili zangu zote na kuanza kuwasaidia wenzangu waliokuwa wameumia.
Tulikuwa saba kwenye gari mmoja alifariki na wengine walikuwa wamevunjika miguu, viuno na viungo mbalimbali.Neno la madhabahuni linatulinda kwasababu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alisema hatutakufa kwa ajali, kweli nimeamini Mungu anatembea na wale wampendao. Wana Efatha hatutakufa kwa ajali sawasawa na Neno la Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat E Mwingira.
WATUMISHI WA MUNGU WALIOTUMWA TABORA KWA KAZI YA MUNGU WASHUHUDIA MATENDO MAKUU YA MUNGU
Mama mmoja alikuwa kichaa akasema yeye anatokea Msumbiji na anaabudu Sabato hawezi kuoka, wakati tunamuongoza sala ya toba akawa anasinzia, alikuwa na irizi kiunoni imefungwa akasema msiifungue, baada ya maombi kukolea akaifungua ile irizi yeye mwenyewe, baada ya kuombewa kumbe ile nyumba wanashiriki mambo ya kichawi na huyu ni mtu wa Uganda akatoa pembe akatupa nje ile irizi na pembe za uchawi na baadaye akaombewa, na tukaichukua ile irizi na vitu vya uchawi tukavichoma moto, ameokoka na anasoma madarasa Efatha.
Kijana mwingine alisema hawezi kuokoka ana dini yake, baada ya kuongozwa sala ya toba akaanza kusema ana mila na desturi zao, baada ya kuombewa akaanza kusema alikuwa anaumwa, kuna siku alikuwa anakunywa maji inzi aliingia kwenye koo aka kaa hapo mpaka sasa anamiaka 7 bila kutoka hapo kwenye koo, akawa anashindwa kula vizuri na kunywa maji.Pia mke wake hazai wala hawana mtoto,baada ya kuombewa na watumishi wa Mungu wa Efatha inzi akatoka katika koo lake, amesimama katika wokovu na anasoma madarasa na mke wake,hivi sasa mke wake ni mjamzito.Anamshukuru Mungu wa Efatha kwa matendo makuu aliyo mtendea.
Dada mmoja anaitwa Asha alikuwa mchawi na baada ya watumishi wa Mungu kumuombea walimchukua na kuishi nae,lakini akajaribu kuwawangia watumishi wa Mungu usiku waka mkamata, alipoendelea kuombewa alikataa kuacha uchawi, Watumishi wa Mungu walimrudisha kwao na kumuonya kama hataki kuacha uchawi atakufa, baada ya siku chache akafa kutokana na nguvu ya Mungu. Kama ilivyo andikwa usimwache mchawi aishi.
SHULE YA WATOTO WADOGO WAKIWA KATIKA IBADA YA JUMAPILI
Katika Picha: Ibada za watoto ambapo watoto hufundishwa kulingana na umri wao, wana waalimu maalum walioandaliwa ili kuwalea na kuwafundisha watoto. Ni vizuri kuwalea watoto katika Mungu ili wawe na msingi mzuri wa Imani. Unapokuja Ibadani na mwanao usihofu wakati wewe ukiwa kanisani, mwanao atakuwa kwenye ibada zao maalum. Karibu sana na Mungu akubariki

Comments