RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAZISHI YA MAREHEMU MAGRETH MKAMA KUFANYIKA JUMAMOSI 28.03.2015 MBAGALA SAKU-DAR

Rumafrica inawapa pole wafiwa wote kwa kuondokewa na ndugu yetu na rafiki yetu Marehemu Magreth Mkama. Marehemu amefariki katika hospitali Muhimbili jijini Dar es Salaam akiwa na tatizo la ugonjwa wa moyo. Siku ya ya Jumamosi 28.03.2015 yatafanyika mazishi eneo la Mbagala Saku jijini Dar es Salaam. Kama ndugu au jamaa unaombwa sana kufika ili kuweza kumuaga ndugu yetu amabye tunaamini hatutamuona tena hapa dunia

Marehem Magreth Mkama alibahatika kuolewa na Bwana Mkama na pia Mungu aliweza kumpa watoto wawili mpaka anapata mauti. Mbali na kuwa katika ndoa pia alikuwa mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania na aliweza kujiunga na kikundi cha THE UNITY FAMILY akiwa kama Katibu na mwimbaji.

Kama waimbaji na wadau wa mziki wa injili Tanzania tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kila jambo analolifanya kwa watu wake hapa duniani. Leo kwa Magreth Mkama na kesho ni kwako, unachotakiwa kukifanya ni kuishi maisha ya kumtukuza Mungu kwani hujui kilicho mbele yako. Mungu azidi kukubariki katika maisha haya ulionayo hapa duniani.

Designed by Rumafrica +255 715 851 523

Comments