RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NABII FLORA PETER: KUJISHUGHULISHA KATIKA KUMTUMIKIA MUNGU

KUJISHUGHULISHA KATIKA KUMTUMIKIA MUNGU
Ukitaka Mungu akutendee unatakiwa kutoa sadaka iliyonzuri katika vitu ulivyo navyo ili kuvunja agano ulikopita ili uweze kupokea. Utoaji ni bora kuliko kitu chochote.

Hakuna kisichoshindikana kwa Mungu, kwa Mungu yote yanawezekana. Ukiamini utatendewa, na ndio maana Yesu aliwaponya watu wenye haja ya kuponywa. Kuna watu wengine hawana haja ya kuponywa bali wapo wapo tu na wanashida nyingi.

Kila mtu ajishughukishe kama vile anamhitaji Bwana. Unatakiwa kujipa muda wa kumuomba Mungu. Huwezi kupokea hata ukiombewa vipi kama wewe mwenyewe hujawa tayari kupokea. Utabaki unasikia tu watu wengine wanashuhudia walivyofanikiwa lakini wewe bado kwasababu hukujishughulisha. Bwana anasema nikaribieni mimi nami nitawakaribia.

Ukiwa mvivu katika kanisa lako utasababisha hata wageni kuwa wavivu. Unatakiwa kujishughulisha ili uwe mtumishi wa watu wengine. Hutabarikiwa bila ya kusogea katika Neno la Mungu. Bwana Yesu aliwaponya wenye haja ya kuponywa. Tunatakiwa kutafuta uso wa Mungu kwanza na kuacha kurukaruka huku na kule.

Wapendwa tusiwe wavivu, Bwana Yesu aliwaponya watu kwa Neno lake. Neno linalohubiriwa kanisani litakuponya na hata sifa zinakufanya ukaribie na Mungu. Ukikaa na muombaji utakuwa muombaji, ukikaa na mpiga domo na wewe utaanza kupiga domo, ukikaa na mtu anayeomba rehema na wewe utatamani kuomba kila wakati.

KUOMBA BILA KUKATA TAMAA
Tusome kitabu cha Luka 18:1-8, akawaambia mfano ya kwamba imewapasa kumuomba Mungu siku zote wala usikate tama. Ikawa Hanna alipodumu kumuomba Bwana Eli alimuangalia sana kinywa chake. Hannaalikuwa akinena moyoni mwake. Hii ni wiki ya maombi na Baraka, hupaswi kukata tamaa, inakupasa kumuomba Mungu siku zote.
Biblia inasema, palikuwa na kadhi mahali Fulani hamchi Mungu wala hajali watu. Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane aliyekuwa akimwendea mwendea, akisema  nipatie haki na adui yangu, alikuwa akienda huko mara nyingi. Naye kwa muda alikataa ma kumfukuza, ondoka unanisumbua ninakazi nyingi za kufanya. Na baadae akasema moyoni mwake kwa kuwa simjali na mtu wala kuwajali watu, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi nitampatia haki yake. Sasa mwambie Bwana unahitaji kupona, mume, mke, chakula. Kumbe unapozidi kuomba kila wakati Mungu anasikia, na ndiyo maana imeandikwa ombeni bila kuchoka nanyi mtapewa, bisheni nanyi mtafunguliwa. Ukinyamaze Mungu hawezi kukutendea. Unatakiwa kuomba kila wakati na Mungu tafanya jambo.

Biblia inasema nikumbushe na tuhojiane, eleza mambo yako upate kupata haki yako. Unatakiwa kufiika kanisa kwako na upate kueleza mambo yako yanayokusumbua. Tunaaambiwa sana kuwa tusikose hata siku moja kumkumbusha Bwana. Mungu akubariki

Comments