RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA CHEMSHA BONGO NA BIBLE -4

ONYO: Huruhusiwi kutumia Biblia kujibu maswali haya, ukifanya hivyo utakuwa umetenda dhambi mbele za Mungu, wala huruhusiwi kuangalia majibu yaliyoandaliwa hapo chini mpaka umemaliza kujibu.
MSIMAMIZI: Roho Mtakatifu na Yesu Kristo
MASWALI YANATOKA  KATIKA KITABU CHA YOHANA 4

Glorymainah- Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania na ni Mwanaushindi

MASWALI.

1. Yesu alipofika katika mji wa Samaria uitwao Sikari, karibu na shamba Yakobo alimpa Yusufu mwanae. Taja jina la kisima kilichokuwepo mahali hapo.

2. Yesu aliomba maji kwa nani baada ya kuchoka pale kwenye kisima cha Yokobo kutoka na safari yake kuwa ndefu, huku akisema, “Nipe maji ninywe”

3. Je, Wayahudi kipindi cha nyuma walikuwa wanachangamana na Wasamaria?

4. Maji ya Yesu ni maji ya namna gani?

5. Kitu gani kinaweza kumtokea mtu ambaye akinywa maji ya Yesu katika maisha yake?

6. Yesu alimwambia nini Yule mjane aliyemuomba maji ya uhai kutoka kwa Yesu?

7. Yule mjane aliyeambiwa na Yesu akamwite mume wake, alimjibu nini Yesu?

8. Malizia semi hii
(a) Nyinyi mnaabudu msichokijua, sisi tunaabudu…………………………..kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi
(b) Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabudio halisi………………………….
(c) Mungu ni……………., nao wamwabuduo yeye inawapasa kumwabudu katika……………………
(d) Nabii hapati heshima katika……………………………………..

9. Masihi ni na nani?

10. Taja eneo au mji amabo Yesu alifanya maji kuwa divai

MAJIBU

1. Yakobo (Yohana 4:6)

2. Msamalia (Yohana 4:7)

3. Hapana (Yohana 4:9)

4. Hai (Yohana 4:10)

5. Hatapata kiu milele (Yohana 4:14)

6. Nenda ukamwite mumeo, uje naye hapa (Yohana 4:16)

7. Sina mume (Yohana 8:17)

8. (a) Tukijuacho (Yohana 4:22)
(b) watamwabudu Baba katika Roho na kweli (Yohana 4:23)
(c) Roho, Roho na kweli (Yohana 4:24)
(b) nchi yake mwenyewe (Yohana 4:46)

9. Kristo (Yohana 4)

10. Kana ya Galilaya (Yohana 4:46)

Comments