RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WANAKWAYA: JOKATE ANATUTIA AIBU

Hamida Hassan
Ile skendo ya kupiga picha za nusu utupu na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii huku midume ikijirushia na kujifaidia kwa macho, ukijumlisha aibu mpya ya kukata mauno mbele ya wanaume, staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amewakera wanakwaya wenzake ambao wamedai kuwa anawatia aibu, Ijumaa lina mchapo kamili.
Staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.

TUJIUNGE KANISA LA SAINT PETER, OYSTERBAY, DAR
Ishu ya Jokate kutupia picha za nusu utupu mitandaoni si mpya, mara kadhaa amekuwa akiripotiwa kwa tabia yake hiyo kiasi cha kuwakera wanakwaya hao wa kanisa analosali la Saint Peter lililopo Oysterbay jijini Dar.
Mbali na picha hizo, safari hii anaandamwa na skendo mpya ya kudaiwa kukata mauno mbele ya midume anapokuwa kwenye shoo zake baada ya kutumbukia kwenye muziki wa Bongo Fleva.

AJADILIWA KANISANI
Kwa mujibu wa baadhi ya wanakwaya hao, wamekuwa wakimjadili mara kwa mara hasa wanapokuwa mazoezini kanisani hapo mara baada ya mmoja wao kurushiwa picha za mwanadada huyo kwenye mitandao ya kijamii.

NI AIBU KWA KANISA?
Baadhi ya wanakwaya hao walikwenda mbele zaidi na kudai kwamba mbali na kuwa ni kioo cha jamii lakini bado ni alama ya kanisa hivyo ni aibu kwa kanisa pia kwa sababu binti aliyelelewa kidini kama Jokate hawezi kuwa na tabia za aina hiyo.


Jokate akiwa kwenye pozi.

AU BIASHARA MATANGAZO?
Kuna baadhi walidai labda mwanadada huyo anafanya hivyo ikiwa ni njia ya kujitangaza yeye na biashara yake bila kujali kama anaweza akajiondolea ute wake na heshima aliyoijenga kwa miaka mingi.
“Ukweli ni kwamba Jojo (Jokate) anatutia aibu maana malezi ya kidini hayapo hivyo. Anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na watu wote.

USHAURI WA BURE
“Sisi tunamshauri arudi awe kama zamani kwani alikuwa binti wa mfano kanisani. Hakuna mtu wa kuonesha maumbile yake muhimu hadharani. Kwanza alipoingia kwenye mambo ya muziki ndiyo hali imekuwa mbaya maana ukiona video zake hutamani kuziangalia na watu wenye heshima zao,” alisema mmoja wa wanakwaya hao kwa niaba ya wenzake huko akiomba chondechonde kutotajwa gazetini.


Mwingine akasema: “Unajua Jokate niliyekuwa namjua mimi siyo huyu, siyo huyu wa kupiga picha hizi chafu, kwa kweli ni aibu kwake na kwetu pia kwani tunaonekana huenda tukiwa kanisani tunaficha makucha yetu, abadilike.”

JOKATE AJITETEA
Akizungumza na Ijumaa juu ya sakata hilo, Jokate alifunguka kuwa, kanisa analosali halimzuii kukata mauno jukwaani kwani anachofanya yeye ni kazi kama kazi nyingine.Jokate ambaye ndiye mmiliki wa bidhaa za ‘brandi’ ya Kidoti alisema kwamba, huwa anakwenda kanisani kama kawaida na kwaya anaimba kama siku zote na hilo haliwezi kumzuia kufanya kazi yake ya muziki na kukata mauno.

MAUNO KWA WINGI YANAKUJA
Jokate alisema kuwa ngoma yake mpya aliyokuja nayo hivi karibuni ya Leo Leo aliyomshirikisha Ice Prince wa Nigeria ndiyo imemdatisha na watu watarajie mauno kwa wingi kwani amejipanga vilivyo.“Mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwani mauno ya sasa si mchezo, ni hatari tupu, nimedata na huu muziki, kiukweli nitajiachia kuliko siku zote,” alisema Jokate ambaye pia ni mwigizaji wa sinema za Kibongo.

Comments