RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ZIMEBAKI SIKU CHACHE KUFIKIA 22 MACHI 2015 GLORIOUS WORSHIP TEAM, KUFANYA MAKUBWA JIJINI DAR

Kla mtu anajua jinsi gani vijana hawa waliojitoa kumtumikia Mungu kwa nguvu zao na mali zao kuhakikisha watu wanaokoka kwa kupitia huduma yao ya uimbaji. Mbali na vipingamizi vinavyojitokeza kama wanadamu, lakini wamezidi kushikana na kufanya kazi ya Mungu. Kikundi hiki ni moja ya vikundi vyenye kukubalika sana na walio wengi kwa uimbaji wao. Mungu amewasaidia kutoa albamu zao kama mbili ambazo zinafanya vizuri sokoni.

Linah Sanga (kulia) akiongea na Sam Sasali juu ya huduma ya GWT

Baada ya kuona Watanzania kuwa na kiu ya kupokea baraka za Mungu kwa njia ya uimbaji, vijana hawa wakaona ni vizuri kufanya tamasha kubwa sana linaloenda kwa jina la SUNDAY CELEBRATION. Katika tamasha hili kutakuwa na maajabu mengi sana ambayo Mungu atakwenda kuyafanya katika eneo la tukio. Watu wataenda kupokea haja za mioyo yao kutoka kwa Baba yetu aliye mbinguni. Unachotakiwa na kuja ukiwa na IMANI kuwa sasa mkombozi wako (Yesu) anakwenda kukuoko. Kutakuwa na waimbaji kama Next Level, Miriam Lukindo, Calvary Band na wengine wengi watakuwepo kuwaunga mkono watumishi wa Mungu (GWT)

Comments