RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHAMUITA YAKONGA MIOYO YA WATU KATIKA KONGAMANO LA WAIMBAJI WA GOSPO JIJINI DAR

Chama cha Muziki wa Injili Tanzania kiliweza kufanya kongamano la waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania kwaajili ya kuliombea Taifa la Tanzania amani na utulifu. Tamasha hili lilihudhuria na watu wengi sana katika kanisa la Pentekoste Light House Christian Center njia panda ya Chuo Kikuu cha UDSM siku ya Jumapili 05.04.2015. Watu waliweza kupokea kile ambacho Mungu aliachilia kwa watu wake siku hiyo ikiwa ni pamoja na baraka za mafanikio, kufarijika, kuponywa n.k.

Katibu Mwenezi wa CHAMUITA, Stella Joel kwa kupitia WATSAP aliwaomba sana waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, wanaposikia matamasha kama haya wasikose kuhudhuria kwani huko ndiko kuna uzima na kutia moyo kama wanafunzi wa Yesu, Tuone baadhi ya picha zilizorushwa katika Group la Watsap la CHAMUITA.
Mada Ruti (kulia) na Sifa John (kushoto)

 Stella Joel -Katibu Mwenezi wa CHAMUITA (kushoto) akifuatia Madam Ruti na Sifa John

Christina Mbilinyi (katikati)

 
Madam Ruti wa Jana Imepita




 Madam Ruti (kushoto) na Lilian Kimola (kulia) wakitokelezea kidogo baada ya kazi ya Bwana


Bishop Dk. Rejoice Ndalima wa kanisa la Pentekoste Light House Christian Center

BONYEZA "Read More" HAPO CHINI KIDOGO KUSHOTO KUTAKA KUONA MATUKIO MENGINE



Comments