RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ERIC JAMES SHIGONGO KUINUA GLORIOUS WORSHIP TEAM (GWT)

Eric James Shigongo ni muumini wa kanisa la WordAlive Sinza Dar es Salaam Tanzania kwa Mchungaji Deo Lubala. Kutokana na juhudi zake za kuchapa kazi bila kuchoka ameweza kumiliki kiwanda cha kutengeneza mageziti ikiwa ni pamoja na magazeti ya udaku katika kampuni yake ya Global Publishers iliyoko Sinza Bamagaga Dar es Salaam. Pia ni mwandishi mzuri sana wa vitabu na hadithi katika magzeti. Huyu ni mtu aliyetoka katika familia ya kimaskini sana na hakusoma ila Mungu aliweza kumuinua kutokana na juhudi zake za kufanya kazi na ubunifu na sasa ni mtu maarufu sana duniani.

Mjasiliamali huyu ni mtu anayependa sana  kujishusha sana umuonapo na hupenda sana kupiga stori na watu wa kawaida sana ukilinganisha na utajiri alionao, na hii imemjengea heshima katika jamii ya Kitanzania na Afrika nzima. Hivi karibunu aliweza kuwaunga mkono vijana wa GWT kwa kuwapa vifaa vya muziki "full" ambavyo vimewasaidia sana GWT kufanya kazi ya Mungu kwa uhuru zaidi ukifananisha na hapo mwanzo walivyokuwa wakiazima kwa watu kwa gharama kubwa sana. Haitoshi, ameweza kuwavuta watu wengi sana kufika katika matamasha yanayofanywa na GWT kwa kuwafundisha jinsi ya kujitoa katika UMASKINI na kuwa TAJIRI. Watu wengi wamekuwa wakifika kumsikiliza na baada ya hapo wanapata burudani ya KIROHO kutoka kwa GWT.

Unaweza kupata badhi ya clips zake kwa KUBONYEZA HAPA au unaweza kutembelea tovuti yake kwa KUBONYEZA HAPA. Mungu akubariki sana

Comments