RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NOEL TENGA KAFIWA NA DADA YAKE: KUAGA MWILI WA MAREHEMU ELITRUDE P. MREMA KATIKA KANISA LA TAG-MWENGE DAR ES SALAAM

Picha na Rumafrica +255 715 851 523
Dada Elitrude P. Mrema mama mwenye mtoto mmoja Glory mwenye miaka 19, siku ya leo ilikuwa ndio siku yake ya mwisho ya kuagwa na wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika kanisa takatifu la Mungu la TAG Mwenge. Watu walikuwa ni mengi sana, na hii inaonyesha ni jinsi gani marehemu alikuwa kipenzi cha watu na jamii kwa ujumla inayomzunguka.

Glory (19) mtoto wa Marehemu Elitrude P. Mrema akiwa na majonzi makali sana

Marehemu Elitrude P. Mrema alizaliwa 26/12/1973 na alibahatika kupata mtoto wa kike mwaka 1996. Marehemu alikuja kugundulika kuwa ana tatizo la apendex na aliweza kufikishwa hospitalini Mwananyamala DSM kwa matibabu na baadaye kugundulika ana upungufu wa damu mwilini. Marehemu alipelekwa katika hospitali ya Jeshi Lugalo DSM na huko wakaona anataizo lingine la kisukari, na siku ya Jumanne 21/04/2015 mnamo saa 8 mchana aliweza kuaga dunia.

Baadhi ya wakilishi kutoka Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania kama Furaha Isaya, Sifa John Lilian Kimora, Magreth Sembuche,  na wengie wengi waliweza kufika. Watangazaji wa vituo mbalimbali vya redio za kidini kama Wapo Redio na Praise Power Radio walikuwepo, nao ni Silas Mbise wa Wapo Redio na Kissaka wa Praise Power Redio. Kulikuwepo na bloggas kama Rulea Sanga wa Rumafrica na wengine wengi. Waimbaji wengine ni Joseph Nyuki aliweza kufika.

Rumafrica inawapa pole wafiwa wote, na jamaa wa marehemu. Tutambue kuwa sisi sote safari yetu ni moja, tutakufa, tunatakiwa kuandaa maisha yetu hapa duniani.

KIPINDI CHA MWILI WA MAREHEMU KUINGIA KANISANI






KIPINDI CHA KUSOMA HISTORIA YA MAREHEMU
Kaka wa marehemu, Noel Tenga aliweza kusoma historia ya dada yake. Hii ilileta simanzi sana kwa walio wengi kutoka na jinsi marehemu huyu alivyokuwa akijituma katika kumtumikia Mungu na pia katika kujibidiisha katika gurudumu la maendeleo. Marehemu ambaye hivi karibuni aliweza kuhamia katika nyumba yake mpya aliyojenga na hakuweza kukaa hata miezi minne akawa anaaga dunia. Unajifunza nini mdau wa blogu hii?
 Noel Tenga
 Noel Tenga

 Mtoto wa marehemu, Glory (19) akifarijiwa na ndugu yake





Mchungaji wa kanisa la TAG Mwenge -Dar es Salaam
Kaka wa marehemu, Noel Tenga akielekea kuketi
 Mtoto wa marehemu Glory (19) akifarijiwa










BAADHI YA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI WALIOWEZA KUFIKA KATIKA MSIBA HUU


Kulia ni Joseph Nyuki, kushoto ni Sifa John


Kulia ni Magreth Sembuche


MATUKIO MENGINE YANAKUJA ENDELEA KU-REFRESH BLOGU HII
------------------------------
KUONA MATUKIO MENGINE BONYEZA "Read More" HAPO CHINI KIDOGO KUSHOTO



KIPINDI CHA KUSIKILIZA NENO LA MUNGU
Mchungaji wa kanisa la TAG aliweza kuhubiri juu ya KUTOTHAMINI SANA MALI KULIKO NAFSI. 
Watu wengi sana wako busy sana katika kutafuta pesa na wamemsahau huyu Mungu. Wanajali sana mali na kusahau kuwa ipo siku watakufa na kuziacha hizo mali zao. Neno la Mungu limekuwa adimu sana vinywani mwao ukifananisha na vile wanavyovisema juu ya utafutaji wa mali. Tukumbuke ya kuwa mali zet tutaziacha hapa hapa duniani, mfano mzuri ni huyu marehemu ambaye alijitahidi sana kutafuta mali na Mungu akamuwezesha kujenga nyumba yake lakini siku ya leo ameviacha na hajui nani atavitumia huku nyuma.

Baada ya ibada kuna baadhi ya watu waliweza kuokoka






Kaka wa marehemu Noel Tenga (kushoto)

KIPINDI CHA MCHUNGAJI WA KANISA LA TAG KUWAITA WATU WANAOHITAJI KUOKOA
Kijana mmoja aliweza kujitokeza na kuweza kuokoka


 





KIPINDI CHA KUAGA MWILI WA MAREHEMU


Kutoka kulia ni mtangazaji wa Praise Power, Kissaka




Joshua wa pili kutoka kulia ni shemeji na marehemu Elitrude Mrema akitokea kanisani




KIPINDI CHA MTOTO WA MAREHEMU, BINTI GLORY (19) KUONA MWILI WA MAMA YAKE KWA MARA YA MWISHO KABLA YA SAFARI KUELEKEA MOSHI KUANZA






Mwimbaji wa nyimbo za Injili na Mkurugenzi wa Sifa Foundation,  Sifa John
Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Magreth Sembuche
 Wa pili kutoka kushoto ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Joseph Nyuki


















Comments