RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SUNDAY CELEBRATION SEASON 5 YA GWT ILIVYOFANA JUMAPILI ILIYOPITA

KIKUNDI cha Kusifu na Kuabudu cha Glorious Worship Team (GWT) Jumapili iliyopita kiliendelea na programu yao ya Sunday Celebration ambayo ilikuwa ni Season 5 katika Ukumbi uliopo Victoria Service Station, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Waimbaji waliofika kuungana na GWT ni pamoja na John Lissu, Emmanuel Mgaya 'Street Pastor' au 'Masanja Mkandamizaji' na The Jordan.

Mbali na waimbaji hao kuipamba siku hiyo, Mjasiriamali mahiri na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo naye alikuwepo kutoa elimu ya ujasiriamali ya jinsi ya kutoka kuwa mwajiriwa hadi mwajiri. Katika somo hilo, Shigongo alitoa nakala zaidi ya 300 ya kitabu chake cha Kutoka Umasikini hadi Mafanikio kwa watu waliohudhuria siku hiyo.

Wiki hii katika Sunday Celebration Season 6, GWT wataendelea kumsifu na kumwabudu Mungu ambapo waimbaji watakuwa The Jordan, GWT wenyewe pamoja na MC Pilipili huku Shigongo akianza somo jipya la ujasiriamali siku hiyo.

Waimbaji wa Glorious Worship Team (GWT) wakitoa burudani katika Sunday Celebration Season 5.




Emmanuel Mgaya 'Street Pastor' au 'Masanja Mkandamizaji' akitoa neo kwa watu waliohudhuria Sunday Celebration.



Kiongozi wa Bendi ya The Jordan, Daniel Mbepera akiimba sambamba na bendi yake.

Eric Shigongo akicheza sambamba na waimbaji wa GWT.

Shigongo akifundisha somo la jinsi ya kutoka kuwa mwajiriwa hadi mwajiri.

Mpiga Saxaphone, Moses Zamangwa akifanya vitu vyake.



Glorious Worship Team Traditional Dancers nao wakionyesha ujuzi wao katika Sunday Celebration Season 5.









GWT wakitoa burudani kwa watu waliohudhuria tukio hilo.

Mmoja wa wadau akifuatilia burudani kutoka kwa GWT.

Comments