RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

EFATHA MWENGE: MFUNGO WA MTEMBEO NA WA KUJIMIMINA KWA BWANA

Rumafrica kwa uwezo wa Mungu iliweza kupata kibali cha kuhudhuria ibada ya Jumapili 03/05/2015 katika kanisa la Efatha kwa Nabii na Mtume Josephate Mwingira. Ibada ya pili ilianza saa 4:00 asubuhi na kumalizika saa7:00 mchana. Katika ibada hiyo nilijifunza MFUMO WA MTEMBEO WA MUNGU NA KUJIMIMINA KWA BWANA. Mahubiri haya yalihubiriwa na mchungaji ambaye sikubahatika kupata jina lake, na hivi ndivyo ilivyokuwa.

Kila mmoja atakaye ingia katika mfungo huo ni lazima apokee mpenyo na kuwekwa huru kama atafuata maagizo yake na maelekezo.

Mama unahitaji mtoto haijalishi una miaka 60 au mayai yamefunga, amini kwa kufunga utapata mtoto.

Kila neno linalotamkwa katika mdhabahu amini linaenda kufanya jambo katika maisha yako. Juhudi zako za kufunga utakutana na majibu ya maswali yako.

SOMO LA MEIMOSI (MARUDIO)


Isaya 28:1-6,
MAMBO MATATU YA KUZINGATIA
1. Kuweka kila aina ya kifungo cha uovu mbali na wewe, kwa mfano kibali chochote/maumivu yoyote

2. Kulegeza kamba za mila, ziwe za mabibi, wazazi au ndugu zako, yale ambayo unapita ambayo wazazi wako wanapitia.

3. Kuacha huru walionewa, kila aina ya mkandamizo uondolewe, chochote kinachoingilia furaha ya moyo wako, ni lazima kupitia mfungo kikaondolewe.

 Weka mwezi huu kuwa wa shukrani. Wachawi, mapepo, chochote kinachokunyima ustawi, kinachosababisha ufanikiwi/kufanya lakini unashindwa, lazima mwezi huu kikashidwe.

NB. Kama utakuwa umefunga na haya matatu hayakutokea, wewe hukufunga bali ulishinda njaa, mwombe Roho Mtakatifu akusaidie kufunga. Hatufungi ili mtu Fulani apone bali tunafunga ili jambo lako litokee, na likitokea uponyaji wako unatokea.

 Tunafunga ili tuzidi kuwa watakatifu wa Mungu. Hakikisha wakati wote unatafakari kama upo sawa na Mungu wako, unapofunga hivyo kila kilichokuwa kinakukandamiza sababu ya ugomvi kikuachilie.
 
 Tunafunga ili kutisha mwili na kuinua nguvu za Roho.  Kwa wale watakao kuwa watii kwa mfungo huu watakuwa na mtaji wa Mungu. Unaweza kuwa na 2,000 na baadae ukapata 2,000,000 kwa sababu una nguvu ya Mungu. Mungu akisema ndiyo hakuna atakayesema hapana.

Jifunze kuchukuwa mahali Baraka zako zilipo, kuna Baraka ziko mahali ili zije kwako lazima uwe na nguvu ya Mungu. Kazana kusikiliza maagizo ya Mungu ya kufunga ili mwili ulegee na Roho iwe na nguvu.  Hakikisha naruhusu wokovu wako udhihirike.

SOMO LA LEO

1 Samweli 1:1-18

Tuombee sana maneno aliyosema mtumishi wake Nabii na Mtume Josephate Mwingira yakaweze kutimia kwako. Ni desturi ya wana wa Mungu kukusanyika kwa pamoja na umoja kwa jambo la Mungu ili kulingana na lile Bwana anataka tunene.

Matoleo ya sadaka ni kitu cha kuunganisha na kile unachoomba, omba Mungu akusaidie katika maombi ya mwezi wa tano kuwa na kiunganishi.  Hannah aliamua kufunga mpaka kile alichokuwa anapitia kueleweka, alimimina moyo wake kwa dhamira mbele za Mungu, hakuweza kushitaki kuwa Peninah amesema mabaya kwake.

 Ukimimina moyo wako mbele za Bwana, na Bwana atatenda tu.  Mungu aliyefanya kwa Hannah ndiye tunayemfuata na kufuata taratibu alizofanya Hannah. Kuhani anashughulikia yote yaliyoshindikana, Eli kuhani alishughulikia na yote yakafanikiwa.

Omba Mungu akutane na haja ya moyo wako. Makubaliano ya Hannah na kuhani yalivyokutana katika ulimwengu jambo lilitokea, na wewe kutanisha kile cha kwako na kile anachokisema kuhani (madhabahuni). Amini kile kinachotolewa madhabahuni, kwa madhabahuni hakuna uongo.

PICHA ZA IBADA YA JUMATATTU INAYOENDELEA KANISANI HAPO
Mwezi huu wa tano, waumini wa kanisa la Efatha wapo kwenye mfungo wa mwezi mzima, ibada zinaendelea kila siku saa  10 jioni kanisani Mwenge.




Comments