RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KIJANA WA RUMAFRICA HAYUKO MBALI NA TAMASHA LA KIMATAIFA LA FLORA MBASHA UBUNGO PLAZA

Mbali na kutengeneza matangazo ya Flora Mbasha juu ya tamasha lake la uzinduzi wa DVD yake ya Nipe Nguvu ya Kushinda na kutambulisha bendi yake inayoenda kwa jina la FLORA MBASHA, Rumafica imeamua kutokosa tamasha hili la kipekee ili isipitwe na matukio yatakayotokea katika ukumbi tulivu wa Ubungo Plaza na kupokea baraka za Mungu kwa kupitia uimbaji wa dada Flora Mbasha. Tamasha hili ambalo litakusanya watu wengi sana na pia watu kwenda kupokea ujumbe wa Mungu kwa kupitia kinywa cha Flora Mbasha.

Tamasha hili litakuwa na waimbaji kama Ambwene Mwasongwa, Edson Mwasabwite, Furaha Isaya, Elizabeth Ngaiza, Tumaini Njole, Madam Ruti na wengine wengi. Mungu meweza kumsadia dada Flora kupata wadhamini wa tamasha hili ambao  ni The Fadhaget Sanitarium Clinic Abra Sound, Wanawake LIVE, Grace Product, AG Press, Gombo Tours, Rumafrica.

Comments