RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NABII NA MTUME JOSEPHATE MWINGIRA-EFATHA MWENGE: MUNGU HANA UPENDELEO



Nabii na Mtume Josephate Mwingira wa kanisa la EFATHA MWENGE- Dar e Salaam Tanzania akiwa katika ibada ya maombi ya jioni tar. 19/05/2015

Rumafrica kwa neema na rehema za Mungu iliweza kufika katika kanisa la EFATHA Mwenge jijini Dar es Salaam na kuhudhuria ibada ya pili iliyoanza saa 4:00 asubuhi siku ya Jumapili 17/05/2015. Nabii Josephate Mwingira ndiye aliyeweza kuhubiri juu ya MUNGU HANA UPENDELEO na HEKIMA. Pia nabii na Mtume Josephate Mwingira aliweza kuwaombea watu ambao wamekosa upendo kutoka kwa Baba zao kutokana kua kufariki, kutokuwa na maelewano kati yao, kufarakana katika ndoa, kutowajua baba zao, kuishi na baba wa kambo na wale wote waliowakosa baba zao kwa sababu mbalimbali. Nabii na Mtume aliwaomba wafike madhabahuni na kuweza kucheza nao na kutamka rasmi kuwa yeye atakuwa baba yao hapa duniani na Mungu ndiye Baba mkubwa.

MUNGU HANA UPENDELEO
Matendo 10:34:35
Mungu hana upendeleo, Mungu hapendelei mtu ila kila mtu amchae anakubalika na Mungu. Huitaji kunung’unika na kulalamika, kuwa Mungu hakupendi.
Ukimtumikia kwa uaminifu anakupa kibali, (Mhubiri 7:12), na unakuwa na ulinzi wa Mungu lakini kama huna hekima huwezi kuona ulinzi wa Mungu na hutapata kibali. Tutajuaje unalindwa na Mungu, ni pale tu maisha yako yanavyokuwa na usalama.
Dalili utakazoziona kuwa uko salama na unalindwa na Mungu ni maendeleo yako kama vile usalama katika fedha zako, kama wewe ni mkulima tutaona mazao yanakaa ghalani, kama mfanyabiashara tutaona mafanikio katika biashara yako, tutaona ukistawi, ukilindwa, na hatutaona ukisukumwa sukumwa.
Unaweza ukawa unampenda Yesu lakini ukawa hufanyi mapenzi yake, na wala hufanyi kwa bidii, ni vizuri sana kufahamu kuwa Mungu hana upendeleo. Unachotakiwa ni kumpenda huyu Yesu na kufanya mapenzi yake kwa bidii.
Kila mtu akifuata taratibu za Mungu ataona mafanikio katika shughuli zake na familia yake inakuwa na ulimzi wa kutosha. Kumcha Bwana ni Hekima, kama unamcha Mungu tutaona hekima na maisha yako yanakuwa na ustawi wa maendeleo.
Tunatakiwa kujifunza Neno la Mungu, na kumjua Mungu wetu,  na kumtambua Mungu anatarajia nini kutoka kwako.
Mungu wetu humbariki mtu yeyote bila kuangalia elimu ya mtu, hutakiwi kudharau nafasi uliyonayo, bali iheshimu sana kwani kuna wengine wanatamani nafasi yako hiyo.
Tambua yakuwa kwa Mungu hakuna shida, na usiseme kwa Mungu kuna taabu, taabu utaweza kupata kama hutamcha Mungu na kutenda haki.
Kumtumikia Bwana ni chanzo cha maarifa, na maarifa huleta fedha, tenda haki kwa kumtumikia Mungu kwa bidii.
SOMO LA PILI: KITABU CHA MTEMBEO
Katika kitabu chetu cha mtembeo wa Mungu siku ya leo tutajifunza juu ya Hekima ambayo mtu anatakiwa kuwa nayo:

HEKIMA
Hekima ni neno zito na zuri, hekima hukusaidia kujua nyakati/muda, na ukijua muda wako unakuwa na uwezo wa kupanga muda wako vizuri kwa kufanya mambo yako. Usipokuwa na hekima na adabu katika kutunza muda wako utaona siku zinaenda na huoni maendeleo wakati wenzako wanasonga mbele.
Sasa jifunze kumcha Mungu ili upate hekima ambayo inakusaidia kutunza muda, na unaweza kufanya vyema na baadaye unapata kibali, na kibali kitakusaidia kufanya vizuri na maovu hayatakutembelea.
Usipokuwa na hekima dhambi inakuandama, usipokuwa na hekima maisha yako yanakuwa ya kubangaiza. Hekima ya Mungu ikikujia kwako unaweza kufanya vizuri na Mungu anakupa Baraka.
Hekima itakuvuta hatua kwa hatua na kukuweka kwenye ufahamu, kumbuka Mungu anasema kabla ya kuwa tumboni mwa mama yako alikujua, na kabla ya kuzaliwa alikutakasa na kukuweka kuwa Nabii wa mataifa. Kila mtu Mungu anakusudi na wewe ili uwe mtu Fulani katika jamii yako na pia kufanya kazi yake.
Unaweza ukawa umeokoka lakini lazima ujiulize, uliokoka ili uwe nani? Roho wa ufahamu anaweza kukufahamisha, jambo unalotakiwa kufanya.
Mungu amekupa mke wako ili awe msaidizi wako na amekupa majukumu ya kuzaa kwahiyo hutakiwi kufanya zinaa, fanya haki yake/ mapenzi yake, unatakiwa kutambua majukumu.
Mtu amchae dunia Mungu anamkubali na kumridhia, na Mungu akikuridhia anafanya maajabu kwako. Mungu hupenda wampendao na utajiri upo kwake, na ile hali ya umaskini inaondoka.
Mungu huwapa watu mali kwa kuwaangalia ni yupi anastaili na yupi hastaili, Mungu anapima matendo mema ya mtu. Kama wewe unatenda mema, Mungu atakubariki na mengi, na kama wewe unatenda maovu basin a Mungu atakuacha kukubariki.
Hata kama ndugu zako/jamaa zako wamekuacha wewe zidi kuchochea vipawa vyako, ipo siku utaona makuu ya Mungu.
Usipendelee wokovu wa mwingine bali jali wokovu wako, wala usitamani upako wa mwingine kwani Mungu hana upendeleo.
MUNGU AKUBARIKI SANA

MATUKIO TA IBADA YA 19/05/2015 JIONI BONYEZA HAPA

Comments