RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA INAMPONGEZA NABII NA MTUME JOSEPHATE MWINGIRA KWA KAZI YA MUNGU ANAYOFANYA NA KANISA LAKE ZIMA

Rumafrica ian kila sababu ya kumpongeza Nabii na Mtume Josephate Mwingira pamoja na  kanisa la EFATNA kwa kazi nzuri wanayofanya ya kumtumikia Mungu kwa akili zao na mali zao. Kanisa limefanyika baraka kwa walio wengi na hasa wale ambao wamewahi kufika katika kanisa hilo na kupata mafundisho ya Mungu  wetu wa mbinguni. Rumafrica imekuwa ikijifunza mambo mengi katika kanisa hilo kutoka kwa waumini, maaskofu, wachungaji, wahudumu pamoja na kiongozi wa kanisa hilo Nabii na Mtume Josepahate Mwingira

Nabii na Mtume Josepahate Mwingira akifundisha siku ya Jumatatu katika ibada ya maombi

Tumefarijika kuona watu wengi sana kutoka kila pande za jiji la Dar es Salaam wakimimika kanisa hapo katika ibada ya maombi inayoendelea katika kanisa hilo kwa muda wa mwezi mmoja.

Siku ya Jumatatu 25/05/205 kanisa hili lilikuwa katika ibada inayoendelea katika kanisa hilo ambapo waumni wote wako katika kipindi cha kufunga kula kwa muda wa mwezi mmoja. Hakika Mungu aliye juu atakwenda kufanya jambo kwa watu hawa ambao wameacha vyakula vyao na kuamua kufunga kula chakula na wengine wameaacha muda wao wa kufanya kazi na kuamua na wakaona kuna umuhimu wa kwenda nyumbani mwa Bwana kusikiliza Neno la Mungu linatoka mbinguni kwa kupitia mtumishi wake Nabii na Mtume Josephate Mwingira.

Huu ni wakati wa kufanya kazi ya Mungu kwani itafika kipindi utashindwa hata kusoma Biblia na utatamani kusoma lakini itashindikana, kuimba, kuhubiri, kushuhudia lakini itashindika kutoka na muda wako wa kufanya hayo yote kuisha. Mungu amekupa muda mzuri sana wa kufanya kazi yake na kuna njia nyingi sana za kumtumikia Mungu. Unaweza kutumia kipaji chako au elimu yako au mali yako kufanya kazi ya Mungu. Baba yetu wa mbinguni amempa kila mtu karama kwa kazi yake. Unachotakiwa kutambua ni kujitahidi kumuuliza Mungu hiyo karama uliyoipata uifanyie nini.

Rumafrica inampongeza mtumishi wa Mungu Nabii na  Mtume Josephate Mwingira alipogundua yeye ameitwa kwa kazi gani, naye aliweza kutimiza lile kusudi la Mungu na kuamua kuanzisha kanisa la EFATHA duniani ambalo kwa sasa linawaumini wengi sana. Mtumishi huyu hajakata tamaa wala kuridhika, bado anazidi kufanya kazi ya Mungu kwa nguvu zake na mali zaje kuhakikisha INJILI inasonga mbele.

Watanzania tunatakiwa kumuombea Mungu mtumishi wa Mungu Nabii na Mtume Josephate Mwingira azidi kufanya kazi ya Mungu na kuzidi kuwaleta watu kwa YESU KRISTO. Ninaamini ukifanya kazi ya Mungu kwa uaminifu, Mungu atakuinua na kukufikisha mahali ambapo hukudhania. Mungu aakubariki sana





Comments