RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SHUHUDA MBALIMBALI KUTOKA KATIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI KWA NABII FLORA PETER

Ibada ya siku ya Jumanne 05/05/2015
NENO LA MUNGU LINATOKA KATIKA KITABU CHA ISAYA 61:1-9
Biblia inasema: Roho ya Bwana ijuu yangu kwasababu Bwana amenitia mafuta, niwahubiri wanyenyekevu habari njema, amenituma ili kuwafungua wale waliovunjia mioyo, kuwatangazia mateka uhuru wao; wewe uliyetekwa na shetani, shetani ameteka afya yako, mafanikio yako, kiroho chako, uchumi wako, ameteka mambo yako hayaendi mbele, Bwana amenituma kuwatangazia uhuru wao waliotekwa.
Biblia inasema: Na hao waliofungwa habari ya kufunguliwa kwao, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika, na kuwafariji wote waliao, kupewa taji ya maua, na furaha badala ya maombolezo; yamkini umefungwa eneo moja ama jingine, umefungwa kifedha, kiroho, umefungwa katika mambo yako, mambo yako hayasongi, umejitahidi sana lakini husongi mbele, nimetumwa kuwafungua wale waliofungwa. Bwana afungue maisha yako leo, aondoe uteka uliotekwa.
Biblia inasema: Kuwaangazia walio katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya taji ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito, wapate kuitwa mti wa haki. Watatengeneza miji iliyoharibiwa, na mahali palipoachwa badala ya vizazi, na wageni watasimama watalisha, nanyi mtaitwa makuhani wa Bwana, mtakula utajiri wa mataifa, na kuusifia utukufu wao, badala ya aibu tutapata mara dufu.

SHUHUDA MBALIMBALI
ANGELA WILLIAM ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA MUUJIZA WA PESA NA PIA KUKU WAKE ALIYEPOTEA AMEMPATA
 
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Angela William
; namshukuru Mungu kupitia sticker ya Fabii Flora, nilizungusha hii sticker ili nipate pesa. Siku ya Jumapili nikaletewa shilingi elfu kumi na leo nimeletewa shilingi elfu kumi.

Vile vile namshukuru Mungu kupitia hii sticker, siku ya Jumamosi kuku wangu nilimnunua miezi miwili iliyopita, jogoo akapotea na Yule aliyekuwa anataga na yeye akapotea. Nilichukuwa sticker nikasema mtu yeyote alichukuwa kuku wangu kupitia hii sticker akakose amani naigeuza hii sticker kuwa kombora, nimekaa kidogo nikaitwa nikaambiwa kuku wako Yule pale na ametotoa vifaranga tisa, namshukuru sana Mungu.
MERYSIANA JOHN ANAMSHUKURU MUNGU NDUGU YAKE KUPONA NA PIA AMEWEZA KUJENGA NI BAADA YA MAOMBI YA NABII FLORA
       
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Merysianna John
; namshukuru Mungu wa Nabii Flora amenitendea mambo mengi sana, kuna ndugu yangu alikuwa amelishwa sumu kwenye chipsi baada ya kuombewa na Nabii amepona, na pia mimi nilikuwa sina hata senti lakini baada ya kuja kwa Nabii Flora nimeweza kujenga na mambo mengine mengi nimefanya, namshukuru sana Mungu.
SUZANA CHACHA ANAMSHUKURU MUNGU MWANAYE KUPONA DEGEDEGE NI BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA
                                Bwana Yesu asifiwe, naitwa Suzana Chacha; namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora kamponya mwanangu, mwanagu alikuwa na degedega ilikuwa inamshika kila wakati, atembea, haongei wala hafanyi chochote, yaani nilihangaika mapaka basi. Lakini namshukuru sana Mungu baada ya kuombewa sasa hivi mtoto wangu anatembea, na anaongea na ile degedege imekata haimshiki tena.
HAMIDA ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA MAOMBI YA NABII FLORA MAADUI ZAKE WAMESHUSHWA CHINI

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Hamida
; Jumapili iliyopita Nabii aliomba kwamba tuna katakata maadui, kazini kwangu nilikuwa na maadui watatu mapaka sasa hivi mmoja kashapigwa yupo chini, namshukuru sana Mungu.

DADA ANAMSHURU MUNGU KWA KUPONA VIDONDA VYA TUMBO NI BAADA YA MAOMBI YA NABII FLORA
Bwana Yesu asifiwe
; Bwana amenitendea, nilikuwa sili na nilikuwa na vidonda vya tumbo, na nilikuwa sili chakula chochote cha kukaanga, lakini baada ya kuja na kumwelezea Nabii Flora,

Nabii akaniombea akaniambia kula kila kitu na wakati huo nilikuwa sijisikii kula naweza nikakaa kutwa nzima bila kula. Lakini kuanzia jana nimekula mpaka najishangaa, namshukuru sana Mungu.
SARA WILLIAM ANAMSHUKURU MUNGU HALI YA MAWINGU NA KIZUNGUZUNGU MBELE YAKE KUTOWEKA BAADA YA KUTUMIA STICKER YA NABII FLORA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Sara Wiliamu
; naishi Salasala, Mungu wa Nabii Flora amenitendea miujiza mingi, nimenusurika kufa wakati nikiwa kazini au nikiwa barabarani. Sasa siku ya jana nimetoka nyumbani naelekea kazini, nimefika mbele kidogo nikataka kugongwa na gari, baadaye nikaendelea na safari, kufika kazini nilipofungua tu geti mbele yangu kukawa na wawingu na kama upinde wa mvua, nikawa sioni kabisa.

Niliingia ndani nikabadilisha nguo lakini bado nikawa naona hali ile ile, nikaenda sehemu nikakaa nikachukuwa sticker ya Nabii Flora nikawa naomba, nikaibandika ile sticker kwenye macho, baada ya hapo ile hali ya kuona mawingu nakizunguzungu ikaisha, namshukuru sana Mungu kwa hilo.

JINSI YA KUFIKA KANISA
Mbezi Salasala-DSM barabara ya Bagamoyo, shuka Mbezi Mbuyuni uliza kanisa la Nabii Flora
Tembelea

Comments