NABII NA MTUME JOSEPHATE MWINGIRA: IBADA RASMI YA KUWAKARIBISHA WALIOZALIWA KATIKA KRISTO

Rumafrica kwa msaada wa Mungu ilibahatika kufika katika kanisa la Mtume na Nabii Josephate Mwingira la EFATH lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam barabara ya Bagamoyo siku ya Jumapili 21/06/2015 . Katika ibada hii ya pili ambayo ilianza saa 4 asubuhi na kumalizika saa 7 mchana ilikuwa ni ya baraka na yenye kuleta matumaini. Nabii na Mtume Josephate Mwingira aliweza kufundisha Neno la Mungu na kuwakaribisha watu waliokoka maeneo mbalimbali kuwa waumini rasmi wa kanisa la EFATHA. Na hivi ndivyo alivyohubiri:

Nabii na Mtume Josephate Mwingira
Leo ni siku njema ya kuwapokea wageni waliookoka na Bwana siku 7/6/2011. Wageni walioweza kukaribishwa katika familia ya Efatha ni wengi sana nah ii inamaanisha kuwa Mungu wa Efatha ni mzuri, anauzika, ni special, ana nguvu ana kila kitu.

Waefeso1:3-7, Tumepewa neema ya wokovu ambayo ni neema ya msamaha, miaka iliyopita Mungu aliona udhaifu wetu na mateso na ndio maana akamleta Emmanuel (Mungu pamoja nasi) ambaye ni Yesu Kristo. Yesu alikuja kuokoa wanadamu ili waweze kufika mbinguni kwa Baba yetu, na Yesu alipowekwa msalabani alilipa madeni yetu yote. Ukikubali kile alichofanyiwa Yesu miaka 2000 msalabani utakuwa umepokea msamaha. Tukikikubali kwa imani zile Baraka za Mungu tunapokea na tunasamehewa dhambi na kuwa Watakatifu.

Kwa nini Mungu anatufanya watu kuwa Watakatifu na anatusamehe dhambi zetu? Kusudi lake-:

Warumi 8:26: Mungu anafanya hivyo ili tuweze kuwa watu wa maombi kwa kupitia Roho Mtkatifu, Roho Makatifu anatuwakilisha kwa Mungu, na kutusaidia kuongea na Mungu, kazi kubwa anafanya ni ku - negotiate na Mungu.

Zaburi 51: Omba Roho Mtakatifu asiondoke Rohoni mwako, kwa sababu anakusaidia kujua nia ya Roho yako, akishaona madhaifu yako basi Roho Mtakatifu hukusaidia kuyapeleka kwa Mungu. Ukiogombana na Warumi 6:28, Mungu anataka upewe mema uwe mtenda kazi pamoja na Yeye, fanya mapenzi ya Mungu ili uweze kufanya kazi pamoja naye. Mema hayo ni Damu ya Yesu inapokuja inaondoa ule wovu na kuwa weupe (Isaya 1:). Ukisoma Isaya1:19 inasema kama utakubali na kutii utakula mema ya nchi, mema ya nchi ya ujana.

Efeso 3:20, Unapata utoshelevu Mungu anaachilia nguvu ya Roho Mtakatifu na unapata kula mema ya nchi. Roho Mtakatifu anakuelewesha ni biashara gani ya kufanya au ni jambo gani la kufanya (Wafilipi 4:4-7) Furahini katika Bwana siku zote, usifurahi kwasababu mtu amekufurahisha, bali furahi katika Bwana siku zote kwa sababu amekupa kibali cha kuwa mtoto wake. Ukiwa na Mungu utashangaa kila kitu kinafanyika, utaona watu wanakuletea zawadi mbalimbali. Mungu anafanya maajabu yake.
Rumi 8:28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

0