MAZISHI YA APOSTLE NA BISHOP JOHN KOMANYA SIKU YA JUMATANO 08/07/2015 KILUVYA GOGONI DAR ES SALAAM: KIPINDI CHA ASKOFU MABOYA KUWASILI ENEO LA MSIBA

Rumafrica iliweza kushuhudia mazishi ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Apostle na Bishop John Komanya aliyezaliwa 1978 mkoa wa Tanga Tanzania akiwa mwanaume wa pekee katika familia yake. Marehemu Apostle na Bishop John Komanya ambaye Mungu alimpa neema ya kufungua makanisa 7 Marekani yanayoitwa Cathedral of Joy na baadae kuja Tanzania kuanzisha huduma hiyo hiyo ya Cathedral of Joy. Huduma yake ilizidi kukua mpaka akaweza kujenga kanisa lake Kiluvya Gogoni jijini Dar es Salaam na kuanzisha bendi yake inayoitwa COJ Band. Marehemu enzi za uhai wake aliweza kufahamika zaidi na watu wengi kutokana na wimbo alioutunga unaoitwa ZAWADI GANI NITAMTOLEA BWANA. Hakika wimbo huu huwagusa watu wengi sana na kujikutana uwepo wa Mungu umewatanda.

Katika watu waliokuwa wanajiibidiisha sana wakiwa bado vijana, hutaweza kumuacha Bishop John Komanya, ambaye kabla ya kifo chake aliweza kufungua kampuni yake inayoitwa JVC lakini ndoto yake iliweza kuzimika baada ya kifo chake. Dakika za mwisho marehemu alikuwa katika mikakati ya kuanzisha mikutano mbalimbali ya kuwatetea walemavu wa ngozi (Albino) na kuliombea Amani na utulivu Taifa la Tanzania ususani kipindi hiki cha Uchanguzi Mkuu wa Urais. Mkutano ambao aliweza kupanga kuuanza ulikuwa ni  wa  mkoani Morogoro siku ya tarehe 26/06/2015 lakini haikuwezekana kutokana na afya yake kutokuwa sawa.


Watanzani waliweza kukusanyika katika kanisa la Cathedraw of Joy ili waweze kumuaga mpendwa wao Bishop John Komanya ambaye alifariki dunia siku ya tarehe 05/07/2015 akiwa na umri wa miaka 37. Baada ya kupata utangulizi sasa naomba uangalie baadhi ya matukio na hasa kipindi cha mtumishi wa Mungu Askofu Datsun Maboya alivyokuwa akiwasili katika eneo la tukio na kuliangalia kaburi kabla ya Bishop John Komanya kwenda kuzikwa.
Kutoka kulia wa pili ni Askofu Datsun Maboya  akifuatia Mch. Lukumayi wa kanisa la Mlima wa Moto

Martha Komanya dada wa Marehemu Bishop and Apostle John Komanya (wa kwanza kulia)
Askofu Datsun Maboya akimfariji dada yake na marehemu Bishop na Apostle JohnKomanya

 Mke wa Mch. Lukumayi (wa pili kutoka kushoto)
 MC Joshua Makondeko akimuomba mama huyu kupiga kigeregere

ENDELEA KUTEMBELEA BLOGU HII KWA MATUKIO MENGIN YA MASIBA HUU
0