RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

R.I.P APOSTLE JOHN KOMANYA...ULIONYESHA BIDII ZAKO KUWALETA WATU KWA YESU

Rumafrica inatoa pole kwa ndugu na jamaa wa Mtumishi wa Mungu marehemu Apostle John Komanya. Tunawapa pole Watanzania na watu wa Marekani ambako mtumishi huyu amewahi kufanya kazi yake ya kumtumikia Mungu. Tulipa pole kanisa la CATHEDRAL OF JOY lililopo Marekani na nchini Tanzania kwa kuondokewa na mwanzilishi wa kanisa hilo duniani. Tunatoa pole kwa bendi yake ya Joy Band ambayo ilikuwa bega kwa bega na mtumishi wa Mungu kwa lengo la kuwavuta watu waje kwa Yesu Kristo.

Apostle John Komanya

Rumafrica imepokea kwa majonzi makubwa sana kwa huyu mtumishi wa Mungu. Tunachokumbuka kutoka kwa mtumishi huyu wa Mungu siku za mwishoni kabla ya kifo chake ni jinsi alivyokuwa anajibidiisha sana kufanya kazi ya Mungu, alikuwa akifika hapa ofisini kwetu kwaajili ya kutengeneza matangazo yake ya matamasha, stickers za mafuta ya upako, mabango, tshirts na vitu vingi sana. Alikuwa ni mtu mwenye kutamani sana kuona kazi ya Mungu inafanyika kwa viwango vikubwa sana, alipenda sana kuona matangazo yake yanakuwa katika viwango vya juu sana. Nakumbuka siki moja tulitengeneza poster yake na yeye hakuweza kupendezewa nayo na kutuambia, naomba ufanye upya kwani huyu naye mtumikia ni mkuu sana, akiona kazi yake iko kwenye kiwango cha chini ataniadhibu, kwahiyo tengeza tangazo upya la kiwango cha juu kwani ni tangazo la Mungu. Kama Rumafrica tulijifunza kitu kutoka kwake na kuona anachosema ni kweli kwani Mungu wetu ni wa viwango vya juu.

Apostle John Komanya alikuwa mtu wa utani
Marehemu John Komanya mabaye alimtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji na kuhubiri alikuwa akifika hapa ofisi kwetu, aliomba sana kusamehewa hataka kama hujamkosea, utasikia anasema, "Kaka naomba unisamehe" huku akicheka. Hakika Rumafrica itazidi kumkumbuka mtumishi huyu wa Mungu. Marehemu alikuwa na ndoto za kufanya matamasha Tanzania nzima na aliiomba ofisi ya Rumafrica kuwa pamoja nayo kwaajili ya kurusha matangazo yake hewani wakati akihubiri, tulipanga kuanza Morogoro tarehe 26/06/2015 na baadae kwenda mikoa mingine kwa kazi ya Bwana.

Apostle John Komanya alikuwa mtu wa utani
Katika watu waliokuwa wanajibidiisha katika kazi ya Bwana, marehemu Apostle John Komanya ni mmojawapo, alikuwa akifika ofisi kwangu hata usiku saa tano kufuatilia kazi zake za matangazo, alikuwa hapendi kuona kazi zake zinacheleweshwa, alikuwa anadiriki hata kutoa pesa zaidi ya ile uliyokubaliana nayo ili kufanikisha kazi ya malengo yake on time.

Kilio chake kingine kilikuwa ni juu ya maalibino, alikuwa anaumia sana kuona walemavu wa ngozi wananyanyaswa na ndio maana aliweza kuandaa mkutano wake wa Morogoro kupata fedha kwaajili ya kuwasaidia maalbino na kupinga unyanyasaji kwa maalbino. Marehemu alikuwa anatamani kuona nchi ya Tanzania inakuwa katika utulivu na amani na pia aliamua kufanya tamasha kubwa kwaajili ya kuliombea Taifa la Tanzania amani na utulivu kipindi cha UCHAGUZI MKUU 2015.

Kuna mambo mengi sana aliweza kuyaongea na Rumafrica ikiwa ni pamoja na kutunga nyimbo za kulisifia Taifa letu na kuhamasisha watu kuwa na upendo. Ukisoma katika sticker yake hapo chini utaweza kujifunza kitu kuhusiana na KIFO CHAKE....

Rumafrica sasa inapenda kukuonyesha baadhi ya kazi za mtumishi wa Mungu Marehemu Apostle John Komanya alizofanya kwaajili ya kumtukuza Mungu na kutangaza Injili

KAZI ALIZOZIFANYA HIVI KARIBUNI NA RUMAFRICA











Comments