RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HALOO....KUNA MAMBO YANATOKEA KATIKA KANISA LA DR. GERTRUDE RWAKATARE HUWEZI AMINI..ANGALIA KILICHOTOKEA JUMAPILI YA 30.08.2014



Ukiangalia kwa makini katika clip hapo juu utaamini jinsi Mungu anavyojidhihirisha LIVE katika kanisa la Mlima wa Moto ambalo limefanyika kimbilio la walio wengi kuja kupokea baraka zao na pia Mungu ameribariki eneo hilo kwa kupitia watumishi wake wenye karama ya kukufanya ufarijike na kusahau mateso yako.

Tunatambua umezunguka maeneo mbalimbali ukitafuta kukombolewa katika shida zako lakini hukubahatika kufika katika kanisa hili la Mlima wa Moto Mikocheni B Assemblies of God. Siku ya leo ni wewe sasa kuamua kuja kushiriki katika ibada za hapa kanisani na pia kushiriki katika ibada za maombezi na uponyaji.

Watu wengi wamepokea baraka zao kama vile utakavyoona katika clip hapo juu. Watu walikuja na mizigo mikubwa ya mateso, lakini walipofika katika kanisa hili, mizigo yao ilishushwa na kuteketezwa kwa moto na sasa wako huru wanafurahia wokovu wao.

Huu sio wakati wako wa kulia na kuteseka bali ni wakati wa kukumbilia kwa Yesu Kristo ili uokolewe na kufurahia maisha yako ya hapa duniani na huko mbinguni.  Nisikuchoshe sana, naomba uangalie hiyo clip hapo juu kujua machahe tu yaliyotokea katika ibada ya Jumapili. Mungu wangu na akubariki sana. Unaweza kutembelea www.mountainofire.blogspot.com kujifunza mengi kutoka katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B Assemblies of God.

Comments