RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO WAKIWA KATIKA MAOMBI MAZITO SIKU YA JUMAPILI 29/11/2015


Ibada hii ilifanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Assemblies of God Mikocheni "B" kwa Askofu Gertrude Rwakatare ambapo waumini wa kanisa hili wakiongozwa na watumishi wa Mungu waliweza kufanya maombi mazito kwaajili ya familia zao na biashara zao. Pia waliweza kupata muda mzuri wa kuliombea kongamano kubwa sana ambalo linategemewa kufanyika siku ya Jumapili 06 hadi 13/12/2015 kuanzia saa 3 asubuhi kwa siku ya Jumapili na katikati ya wiki litakuwa likifanyika saa 10 jioni. Maombi haya yaliweza kuchukua muda mrefu kuhakikisha kuwa Mungu analibariki hili kongamano la Shiloh Tanzania 2015 ili likafanyike baraka kwa watu watakaofika siku hiyo.

 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.
Konagamno hili ambalo hufanyika mara moja tu kwa mwaka kwa muda wa siku 8 tu katika kanisa hili la Mlima wa Moto Mikocheni "B" limeweza kuleta matunda mema sana kwa watu waliobahatika kufika katika maisha yao. Siku hizi za kongamano utaweza kusikia shuhuda mbalimbali za watu waliobahatika kufika katika makongamano yalioyopita.

Kutakuwa na waimbaji mbalimbali kama vile Bahati Bukuku, Alice, Gideon Mutalemwa, Goodluck Gozbert, Vocal Akapela, GWT na wengine wengi. Kutakuwa na wahubiri kama vile Mch. Noah Likumai, Mch. Karisto Kyando, Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Bishop Dustan Maboya na wengine wengi.

Jinsi ya kufika panda magari yatakayokufikisha Mwenge mataa, uliza watu wa babaji wakupeleke kanisani kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.

Ukitaka kujua mengi kuhusu hudma hii tembelea
www.mountainoffiretanzania.blogspot.com.
Facebook: Mountainoffire Tanzania










Comments