RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

DK. SHEIN KUAPISHWA LEO


Dk. Mohammed Shein

ZANZIBAR: Rais Mteule wa Zanzibar Dk. Mohammed Shein aliyeshinda uchaguzi wa marudio uliofanyika Jumapili iliyopita, ataapishwa leo katika Uwanja wa Amaan mjini Unguja.

Katika tukio hilo la kihistoria, viongozi mbalimbali wa kitaifa wanatarajiwa kuhudhuria wakati rais huyo wa awamu ya saba akiapa kuanza awamu yake ya pili ya uongozi wa taifa hilo lenye visiwa viwili vya Unguja na Pemba.

Rais Shein alishinda uchaguzi huo wa marudio, kufuatia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana kwa kile alichodai kuwepo kwa dosari kutoka kwa baadhi ya vyama vilivyoshiriki uchaguzi huo.

Hata hivyo, baadhi ya vyama vya siasa vikiwemo Cuf na ACT-Wazalendo vilisusia uchaguzi huo.

Comments