RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

GARI LINALOJIENDESHA LA GOOGLE LAGONGA BASI



MOJAWAPO ya gari la Google linalojiendesha limegonga basi moja mjini California, Marekani mwezi uliopita. Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Sio mara ya kwanza kwa gari linalojiendesha la Kampuni ya Google kuhusika katika ajali, lakini huenda ni mara ya kwanza kwa magari hayo kufanya ajali.

Kampuni ya Google inatarajia kukutana na idara ya magari mjini California ili kuzungumzia kuhusu ajali hiyo na kubaini ni nani wa kulaumiwa.



Mnamo Februari 14, mwaka huu gari hilo ambalo lilikuwa likisafiri kwa kasi ya kilomita 3 kwa saa liligonga basi moja la umma lililokuwa likisafiri kwa kasi ya kilomita 24 kwa saa.

Mtu aliyekuwa katika gari hilo la Google aliripoti kwamba alidhani basi hilo lingepunguza mwendo ili kuisubiri gari hiyo kupita hivyo basi hakuingilia kompyuta inayoendesha gari hilo.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Mountain View karibu na makao makuu ya Kampuni ya Google.

Katika taarifa yake Google ilisema “Tunabeba lawama kwa sababu iwapo gari letu lisingeenda kusingekuwa na ajali”

Comments