RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KAHAMA WAMTAKA PROFESA MAKAME MBARAWA PASAKA


Upendo Nkone ni mmoja wa wahudumu katika Tamasha la Pasaka Kanda ya Ziwa.
Na Mwandishi Wetu 

Wakazi wa Mji wa Kahama wamemkaribisha kwa mikono miwili, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kwenye Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi 28 mjini humo. 

Wakazi hao ambao hawakujitambulisha majina yao walieleza kwamba Profesa Mbarawa ni Waziri ambaye walikuwa wanamhitaji wajumuike naye pamoja ili kufikisha ujumbe wa Neno la Mungu kama maandiko matakatifu ya Mungu yanavyoeleza kwamba wakutanapo wawili kwa jina langu, nipo katikati yao.

“Tamasha la Pasaka si la kidini kinadharia kwa sababu, michango inayopatikana kupitia viingilio hayachagui, dini, jinsia wala kabila, hivyo wakijumuika naye itasaidia wakazi wa mikoa hiyo kupona kupitia maandiko matakatifu,” alisema mmoja wa wakazi wa mji huo maarufu kibiashara. 

Walisema watashukuru wakijumuika na Waziri Mbarawa kwa sababu italeta chachu ya ibada hiyo takatifu ambayo uwasilishaji wake unafanyika kupitia nyimbo za Injili na maombi kutoka viongozi wa dini. 

“Kwanza tunashukuru kwa Kampuni ya Msama Promotions kutuletea Waziri Mbarawa kwenye Tamasha la Pasaka, kuja kwake kutasaidia kukemea machafu yaliyokuwa yakifanyika Kanda ya Ziwa kwa mauaji ya Vikongwe kwa imani za kishirikina na walemavu wa ngozi ‘albino’,” alisema mmoja wa wakazi wa Kahama. 

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema hivi sasa Kamati yake inaendelea na mchakato wa kufanikisha tamasha hilo. 

Msama alisema waimbaji watakaopanda jukwaa la tamasha hilo wanaendelea kujifua vilivyo kwa lengo la kufanikisha kazi hiyo ya Mungu. 

Tamasha la Pasaka linatarajia kuanza Machi 26, mkoani Geita kwenye ukumbi wa Desire, Machi 27 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na kumalizia Uwanja wa Taifa mjini Kahama.

- See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2016/03/kahama-wamtaka-profesa-makame-mbarawa.html#sthash.JmCPmHBj.dpuf

Comments