MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MATUKIO YA IBADA YA UFUFUO SIKU YA PASAKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" JIJINI DAR ES SALAAM - TANZANIA

Siku ya Jumapili ya Pasaka 27.03.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" linaloongozwa na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kulifanyika ibada ya UFUFUO ya kusherekea ushindi wa Bwana wetu Yesu Kristo alioupata miaka mini iliyopita kwa kufufuka kwake. Kifo cha Bwana wetu Yesu Kristo kilisababisha wanadamu kukombolewa na vifungo vya shetani. Bwana wetu alikufa kwasababu ya dhambi zetu, aliweza kusulubiwa, kupigwa, kutemewa mate, kutukana, kudharauliwa na kuzikwa kaburini ili mimi na wewe tuwe huru.
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Tunamshukuru Mungu ibada iliweza kutufundisha jambo juu ya ufalme wa mbinguni na kuzidi kumtumikia Mungu. Wachungaji wetu waliweza kutukumbusha mambo mengi ambayo yalifanya imani zetu kuuwishwa tena. Tulikumbushwa kuzidi kumtumikia Mungu na kuwa watakatifu tusie penda kufanya mabaya na pia kutii maagizo ya Mungu kupitia watumishi wake na kusoma kitabu kitakatifu yaani Biblia (kufuata yale yaliyoaandikwa katika Biblia)
Mlima wa Moto Praise and Worship Team

Ibada hii ilihudhuriwa na watu wengi sana kutoka kila pande za jijini la Dar es Salaam waliofika kwaajili ya kupata Neno la Mungu kutoka kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na wachungaji wengine wa kanisa la Mlima wa Moto.
kulia ni mama Mushobozi

Katika ibada hii kulikuwa na waandishi wa habari waliofika kwaajili ya kupata habari za Mlima wa Moto kutoka kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, na pia kupata ule ujumbe ambao Mungu amempa Bishop kwaajili ya kuwaambia Watanzania na dunia nzima kuhusu Pasaka. Waaandishi wa habari waliweza kufika katika ofisi ya Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na kuongea naye.
Watu wengi sana waliweza kuokoka na kujiunga na kanisa hili la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Hii inatokana na jinsi watu wanapopokea mahubiri ya Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kufika kanisani hapo au kwa kusikiliza Praise Power Radio au kwa kuangalia kipindi kinachorushwa Channel 10 kila siku ya alhamisi saa 3:30 usiku. 
Ujumbe wa Bishop mara nyingi umekuwa ukigusa maisha ya watu wa rika zote na umefanyika faraja kwa walio wengi. Mungu amempa neema ya pekee sana Bishop huyu kwa kukubalika na jamii ya Watanzania kutokana na jjuhudi zake za kuhakikisha injili inasonga mbele na watu wanafanikiwa Kiroho na Kimwili.
Kuna baadhi ya watu walitokwa na mapepo wakati wa maombezi yaliyokuwa yakifanyika katika ibada hii ya Mlima wa Moto. Watu wenye shida mbalimbali waliweza kufunguliwa na kuwekwa huru banda ya wachungaji na watumishi wa Mungu walipoanza kushambulia kazi za shetani kwa maombi. watu walipiga kelele na wengine kugaragara chini wakihangaishwa na nguvu za giza.

Praise & Worship Team ilifanyika baraka sana katika ibada hie, kupitia uimbaji watu walianza kupokea Roho Mtakatifu na wengine wakaanza kunena kwa lugha hasa katika kipindi cha kuimba nyimbo za kuabudu zilizoongozwa na Mch.Prisca Charles wa Mlima wa Moto Mikocheni "B". 

Hakika Mungu anawatumia vijana hawa kwa njia anayoijua yeye kuhakikisha watu wake wanapona kwa kupitia nyimbo zinazoimbwa kupitia vinywa vyao. Tunatambua Mungu wetu anapenda sana kuona watoto wake tunachukua muda kwaajili ya kumsifu na kumwabudu kupitia nyimbo, na ndio maana waimbaji wa Mlima wa Moto wametambua hilo na sasa wameweza kufika mbali katika uimbaji wao kwasababu wanamuimbia ni mkubwa kuliko chochote hapa dunia.
Nikualike sana wewe ambaye hukubahatika kufika katika ibada hii ya Jumapili ambayo mara nyingi huanza saa 3 asubuhi kila Jumapili, sasa ni wakati wako wa kuchukua maamuzi sahihi ya kufika kanisani Jumapili ya wiki hii ili uweze kupokea kile kitu ambacho Mungu alikuandalia ukipokee kupitia Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Ninakuombea Jumapili nikuone katika ibada hii.
Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia katika kituo cha mabasi cha Makumbusho jijini dar es Salaam, nje kidogo ya kituo hicho utaona magari ya Mlima wa Moto, ingia humo na hakuna atakayetaka nauli yako au fika Mwenge kwenye mataa utaona watu wanasema "Kwanisani kwa Mama Rwakatare), ingia humo ndani. Nikutakie siku njema

BONYEZA "Read More" HAPO CHINI KIDOGO KUSHOTO KUONA MATUKIO MENGINE YA IBADA HII YA UFUFUO MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" Mch. Prisca Charles
 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiwa katika maombezi

 Mch. Francis Machichi


 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiombewa na pia wakimuombea yeye na famili yake

 Waaandishi wa habariWALIOKOKA JUMAPILI YA PASAKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B
Mch. Francis Machichi akiwaongoza sala ya toba waliokoka na kujiunga na kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

0