MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MGANGA WA KEINYEJI KASIMU ALIYETAKA KUMPINDUA BISHOP GERTRUDE RWAKATARE AJISALIMISHA KIZANI GEZAULOLE KIGAMBONI DAR

Mganga mkuu wa eneo zima la Kigamboni Bwana KASIMU siku ya Jumapili 28.02.2016 aliweza kunyoosha mikono yake baada ya kushindwa kumloga Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiwa mkutano Kizani Gezaulole Kigamboni jijini Dar.

Bwana Kasimu kabla ya mkutano wa Injili wa siku 8 za miujiza ulioandaliwa na kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B kwa lengo la kuwaombea wananchi wa Kigamboni na kufungua rasmi kanisa jipya la Mlima wa Moto Kizani Gezaulole Kigamboni, alisikia gari likitangaza kuwa kutakuwa na mkutanoo mkubwa wa Injili karibu na eneo analoishi Kizani. Kasimu aliweza kuchukua kipeperushi kilichokuwa kinagawiwa na watumishi wa Mungu wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Nas aliposoma aliona mhubiri mkuu atakuwa ni Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Kitendo cha kusikia sauti ya watumishi wa Mungu waliokuwa wakitangaza kwenye gari ya kuwa "Waganga wataacha uganga wao na wataokoka na wasipofanya hivyo watakufa" Kasimu alichukua sana na hayo maneno na akaanza kujipanga sasa kumuangamiza kiongozi wa kanisa hilo ambaye ni Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Mkutano ulipoanza siku chache, aliweza kufika katika mkutano huu akiwa amebeba silaha za kumuangamiza Bishop na kumuabisha mbele za jukwaa. Bishop alipowasili aliweza kupanda jukwaani kwa kazi ya Mungu.

Kasimu akaanza kazi yake ya kutaka Bishop asiweze kusimama kwenye kiti alichokalia, na alipojaribu kutumia silaha yake aliyokuja nayo akashangaa Bishop kasima tena bila ya hofu, kitendo hicho kilimuudhi sana na akajaribu kwenda kuchukua silaha nyingi, nayo ikashindika, akachukua viyoo viwili navyo vikapasuka. Alivyoona hivyo Kasimu akasema kuanzia sasa anaokoka kwani Bishop ana Mungu wa kweli.

Kumbuka huyu ni mganga mkubwa sana na ana waganga wadogo zaidi ya 20 wanaomtegemea, na dawa alizokuwa akitumia zina gharama wa milioni 15 hivi.

Kabla hajaamua kuokoka ilikuwa ngumu sana kwake kuokoka kwani alikuwa anaogopa ataishije na itakuwaje kwa wateja wake ambao wanamtegemea na amechukua fedha zao, lakini mchungaji Dickson wa kanisa la Mlima wa Moto alivyokaa naye na kuongea naye kuhusu habari njema za Mungu kwa upole na utaratibu, Kasimu alioweza kuguswa na nguvu za Mungu na kuamua sasa kuokoka kwani aliamini kuwa kanisa la Mlima wa Moto lina Mungu wa kweli kwani kwa uganga wake wote ameshindwa kumloga na kumuabisha Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.

Hii nistory fupi tu lakini utaona katika clip inayoandaliwa kwa sasa.

Kasimu aliomba sana ulinzi kwani alisema kwa sasa anajua kuna watu watakuja kumtishia na wengine kumfanyia fujo kwa kutotimiza maagano walioagana. Na kipindi watumishi wa Mungu wanakwenda nyumbani kwa Kasimu waliweza kumuona mganga akiwa ametoka kwa Kasimu na kumuomba aachiwe uganga na asiuunguze na pia aliweza kutoa maneno ya kumtishia maisha kwanini ameamua kuwasaliti...!!

Nisikumalizie uhondo kesho clip itakuwa hapa hapa utasikia..Tumuombee Bishop Dr. Gertrude Rwakatare...Nisamehe kama nimekosea typing

MSIKILIZE HAPA


 Ksimu nyumbani kwake akielezea alichokifanya

 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare (kulia)


 Kasimu akionyesha dawa aliweka mlangoni kwaajili ya kuvunja nguvu za watu wanakuja kwake kwa lengo baya

0