RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PICHA 3: RAIS MAGUFULI LEO KAENDA KUMJULIA HALI MAALIM SEIF BAADA YA KUPATA TAARIFA ZA KUUGUA KWAKE


President wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuliamemtembelea na kumjulia hali makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad kwenye hoteli ya Serena Dar es salaam ambako anapata mapumziko baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Hindu Mandal alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Pamoja na kumpa mkono wa pole, Rais Magufuli amemuombea Maalim Seif Shariff Hamad kupona haraka ili aweze kuendelea na shughuli zake kama kawaida na kuyasema haya >>> ‘Nilishtushwa sana na taarifa za kuugua kwako lakini sasa nafurahi kukuona ukiwa mwenye afya nzuri ikilinganishwa na taarifa nilizozipata hapo awali, nakupa pole sana”

Kwenye taarifa iliyotumwa na Ikulu kwa millardayo.com , Maalim Seif Shariff Hamad amemshukuru Rais Magufuli kwa ukarimu na upendo aliouonesha kwa kumtembelea hotelini hapo na amewahakikishia watanzania kuwa hali yake sasa inakwenda vizuri na inazidi kuimarika kila kukicha.

“Sasa hivi ninaweza kutembea vizuri, kufanya shughuli zote mwenyewe bila ya msaada wa mtu yeyote yule, na ni matumaini yangu kwamba baada ya muda mfupi, hali yangu itarudi kama kawaida, nije nishirikiane na watanzania wenzangu katika kutekeleza majukumu ya nchi yetu“ Maalim Seif alimweleza Rais Magufuli.

Maalim Seif alipatwa na kizunguzungu kikali akiwa uwanja wa ndege Zanzibar akielekea Dar es salaam juzi ambapo ilibidi aombe msaada wa watu kumsaidia kupanda ndege, alipofika Dar na kulazwa Hospitali uchunguzi ulionyesha hakuwa na tatizo lolote bali ni uchovu tu.

Comments