RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PICHA: MATUKIO YA WAUMINI WAPYA WA KANISA LA MLIMA WA MOTO WAKIBATIZWA SIKU YA JUMAPILI 20.03.2016 JIJINI DA RE SALAAM

Hakika Mungu anazidi kuwaokoka watu kupitia huduma ya Mlima wa Moto Mikocheni "B". Tuna kila sababu ya kusema asante Mungu kwa huduma ya Mlima wa Moto kwa kufanyika chombo au daraja ya kupitisha watu kuja kwako Mungu. Kupitia watumishi wako unawatumia kama chombo chako kufikisha ujumbe wako kwa wanadamu.

Jumapili hii 20.03.2016 tumeona ukiwagusa watu kwa njia ya tofauti sana na wengine wakaamua kuokoka na kukurudia wewe Bwana. Hakika Mungu tunafarijika sana na wema wako kwetu. 

Kuna watu umewatoa katia starehe zao za dunia na ukaamua kuwaleta kwako kwa kupitia huduma yako hii ya Mlima wa Moto. Tunakuomba sana Mungu wetu uzidi kuwalinda hawa waliokoka siku hii na kubadilisha maisha yao kuwa bora ili wakafanyike ushuhuda kwa majirani zao, marafiki zao na ndugu zao. Kawalinde na mabaya yasiwapate na wakafanyike kivutio kwa wengine kutamani kuokoka..

Mungu ibariki huduma ya Mlima wa Moto ili iendelee kukua na kubadilisha mioyo ya watu ikutamani wewe Mungu wetu.

Tumeona Mungu watu wakifunguliwa katika n=bahari ya hindi Mikocheni "B" wakati wakibatizwa na watumishi wako uliowachagua kwa siku ya Jumapili kufanya kazi yako. Tumeona wenye mapepo wakitokwa na mapepo na wenye shida mbalimbali ukiwapa kile wanachokihitaji. Ubatizo huu umewasababishia kuitwa sasa KIUMBE KIPYA na wamesahau ya kale na sasa wanaendelea na maisha mapya yenye matumaini mema..

Tunakushukuru Mungu wetu..Amen

 Wakiwaelekea kwenye basi tayari kwa safari ya kwenda baharini kubatizwa
Wakiingia kwenye basi, safari kuanza 


 Basi la Mlima wa Moto Mikocheni "B" likiwa na waumini wapya, tayari kwa safari ya baharini kubatiza
 Wakiwa katika eneo la tukio, wakisubiri Mlango wa Beach kufunguliwa
 Wakielekea baharini kubatizwa

 Wabatizaji wakitafuta mahali pazuri pa kubatizia na kuwaombea waumini wapya hawa
 Kabla ya Ubatizo ilikuwa ni kuimba na kumsifu Mungu

BONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KIDOGO KUSHOTO






 Baada ya kubatizwa ni maombi







Picha zimepigwa na Rumafrica +255 715 851 523

Comments