RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TUJIKUMBUSHE KIDOGO: M HE. PAUL MAKONDA AMSHUKURU MUNGU KUMUWEZESHA KAZINI


Mh. Paul Makonda akiwa na Mke wake akimshukuru Mungu

Mhe. Paul Makonda siku ya Jumapili alikuwa anatimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe kuwa mkuu wa Walaya Kinondoni,asubuhi ya leo katika Ibada Kanisani Living Water Center Ministry Kawe alipolelewa kiroho na anapo abudu alikuja kumshukuru Mungu na kutoa sadaka ya shukrani kwa hatua ambayo amefika.

Katika Ibada hiyo Mh Paul Makonda aliongozana na mke wake; alipopewa kuzungumza alisema anamshukuru Mungu kwa kutimiza mwaka tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Wilaya Kinondoni akisema haikuwa rahisi kwake ila Mungu amemuwezesha. Makonda aliongeza kwa kusema "usishindwe kufanya mambo ya kimaendeleo kwa changamoto za kimazingira au chochote kama kwangu ambavyo imekuwa ikionekana"


Mapema akimkaribisha kuzungumza Mhe. Paul Makonda Kiongozi wa Kanisa hilo Apostle Onesmo Ndegi alikuwa anaelezea jinsi ambavyo amemlea kiroho Mh.Makonda hata kabla ya kuingia kuwa mtumishi wa serikali jinsi alivyokuwa mbunifu wa shughuli mbalimbali hivyo kinachofanyika leo sio kipya kwake.


Baada ya Ibada hiyo ya shukrani Bwana akatenda zaidi kwa kumfanya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.


Hongera Paul Makonda kwa kuteuliwa kuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Comments