RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WAOKOVU WAPYA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI 13.03.2016

Siku ya Jumapili 13.03.2016 Rumafrica iliweza kuhudhuria ibada ya Jumapili 13.03.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Ibada ilikuwa na upako wa aina yake kuanzia kipindi cha maombi, sunday school na Ibada kuu. Katika kipindi cha Sunday School  kilichoongozwa na Mch. Elizabeth kuna baadhi ya watu waliweza kuokoka na kujiunga rasmi na kanisa hilo. Waumini hao wapya waliombewa na Mch. Otieno na baadae kupelekwa baharini kwaajili ya ubatizo wa maji mengi. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuawaandalia vinywaji waokovu hawa wapya ndani ya kanisa la Mlima wa Moto.
 Kama Wakristo wa Mungu tunajukumu kubwa sana kwaajili ya kuwaongoza hawa waumini wapya ili wazidi kusonga mbele. Kama tunavyojua ya kuwa shetani hatamani kuona watu wanaokoka, ila anatamani kuona watu wanakuwa chini yake ili awatumikishe anavyotaka, kwahiyo unapoona mtu kaokoka ujue ni kwa neema ya Bwana na mtu huyo anahitaji usimamizi mkubwa sana kipindi hiki cha kwanza ili imani yake iimarike na baadae kujitegemea kama Mkristo imara.
 Tunamponeza sana Bishop Gertrude Rwakatare kwa maono yake ya kuanzisha hili kanisa ambalo limefanyika baraka kwa Watanzania na watu wanaofika kuabudu mahali pale. Watu wamekuwa wakiingia kanisani wakiwa hawana fedha, maisha yao magumu, wanaumwa, wameumizwa lakini wanapokanya kanisa hili na kuishi kama vile Yesu anavyotaka wamekuwa wakibarikiwa na wamekuwa wakishuhudia mengi jinsi Mungu alivyowatendea.
Kwahiyo tunakuomba sana kutenga muda wako kwaajili ya kuwaombea hawa ndugu zetu ili wasikate tamaa na kurudi katika maisha ya zamani ya kuteseka. Tunatakiwa kuonyesha moyo wa upendo na kuwasaidia pale wanapohitaji msaada wako. Waumini hawa wanakutegemea wewe kama Mkristo uliyekomaa kuwafundisha na kuwaonyesha njia sahihi ya kwenda mbinguni.

 Kuna baadhi yao pengine walikuwa ni watu waliokataliwa na ndugu zao au marafiki zao, sasa wanapokuja kwetu tuliokoka tusiwatenge kwani wametoka baadhi yao kutengwa. Utawafanya washindwe kujua Mungu ni nani na Shetani ni nani, kwasababu wewe uliyeokoka huonyaeshi matendo ya Mungu ya kupendana na kuhurumiana. Mungu akubariki sana
 Waokovu wapya wakiwa wameshika fomu za kujiunga rasmi na kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"
 Mch. Francis Machichi akiwaombea….
Baadhi ya waokovu wapya wakiwa wamelala chini wa kilia baada ya kombewa na kuguswa mkono na wachungaji wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Comments