MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

ALIYEMTUKANA RAIS MAGUFULI KWENYE FACEBOOK KAPATA DHAMANA


Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imempa dhamana Mtuhumiwa Isaac Abakukianayetuhumiwa kumtukana Rais John Magufuli kupitia kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

Hakimu mfawidhi Agustino Rwezire amesema Mahakama baada ya kupitia hoja mbili zilizotolewa na upande wa mashtaka na mshtakiwa, imeridhia kutoa dhamana kama haki ya msingi ya mshtakiwa kutokana na kosa alilotenda ambapo dhamana hiyo ni ya Wadhamini wawili waliotakiwa kuwa na jumla ya shilingi milioni tano.
Kwenye siku ya kwanza kufikishwa Mahakamani Polisi walisema Tarehe 17 March 2016 Isaac Abakuki akiwa nyumbani kwake Olasiti Arusha alipokea ujumbe kwenye account yake ya Facebook ukisema ‘mnamlinganishaje Magufuli na Nyerere’ ukiwa ni Ujumbe wa mjadala ulioanzishwa kwenye mtandao wa kijamii kufuatia hatua ya Rais Magufuli kupiga simu kwenye kipindi cha Clouds 360 CloudsTV na kuwapongeza Watangazaji wa kipindi hicho.
0