RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

APONA KIDONDA CHA MGUUNI, MGUU WAPONA KUKATWA BAADA YA MAOMBEZI YA MCH. NOAH LUKUMAY SIKU YA 10.04.2016 MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"


Katika Ibada ya Jumapili 17.04.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” jijini Dar es Salaam, mama huyu aliweza kumshukuru Mungu kwa kupona kidonda kikubwa katika mguu wake baada ya kufanyiwa maombi siku ya Jumapili 10.04.2016 na hivi ndivyo alivyoshuhudia,
“Bwana Yesu asifiwe sana. Jamani nimeuona mkono wa BWANA, kwa sababu nilikuja hapa kanisani mguu wangu ukiwa umepasuka pasuka, umevimba, unauma, unatoa usaa na maji na siwezi kutembea kabisa. Nimezunguka katika mahospitali mbalimbali, nimefanyiwa vipimo mbalimbali na ilifika kipindi nikalazwa katika hospitali ya Amana. Madakytari wa AMmana walishindwa kunitibu wakanipa rufaa ya kwenda hospitali ya Mhuhimbili, na nilipofika Muhimbili, Daktari akaniambia watachukua vipimo vingine halafu baada ya siku chache niende nikachukue majibu.


Nikamua kufika kanisani siku ya KUFUNGULIWA KWAKO (Deliverance day) na nikamkuta Mch. Noah Lukumay akiombea watu, nikajipenyeza madhabahuni niombewe na yeye akaniombea. Siku Jumapili 10.04.2016 nikaja kanisani nikaombewa na Mch. Noah Lukumay. Bandeji ya kidionda ilidoka hapa kanisani. Siku ya Jumatano nilikuja tena kanisani kwa maombi ya deliverance, kuanzia hapo mguu ukapona. Madaktari walikuwa wameshaniambia kuwa una tatizo kubwa mguu unaweza ukakatwa kabisa, lakini MUNGU amenitetea jaman. Namshukuru MUNGU sana na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare nakushukuru sana, watumishi wote, akina mama na kanisa zima nashukuru wahudumu kwa upendo kwani nilipokuwa naumwa walikuwa wakiniuliza naendeleaje..!! Leo hii ni mzima. Asanteni














Comments