RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

AYO.com: HABARI 5 KUBWA KWENYE TV ZA TANZANIA APRIL 27 2016

Kama utakua ni mpenzi wa kutazama taarifa ya habari na hukupata time ya kutazama taarifa ya Habari April 27 2016 kupitia TV za Tanzania usijalimillardayo.com imekurekodia habari 5 kupitia TV za Tanzania.


Habari kutoka Channel 10…Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka BRT

Watumiaji wa barabara watakiwa kuzingatia sheria za usalama barabrani ‘Hilo swala la watu wasio husika na miundo mbinu kutumia miundo mbinu, hiyo ndio hadha na kero ambazo tulizonazo sasa hivi kwa siku nne tu zilizopita tayari magari yetu ya mradi yameshakwaruzana na watu wasiopaswa kutumia barabara hizi‘>>>Msemaji wa UDA RT


Habari kutoka Clouds TV…Ustawi wa Watoto Upo API
Walimwengu wanasema mtoto umleavyo ndio akuavyo iko wapi mantiki ya wazazi wanaowarekodi watoto wao, ‘Watoto wanavyofundishwa kitu chochote au wakafanyiwa matendo fulani yanaganda kwenye ubongo wao mpaka ukubwani kwao‘>>>Mwanasaikolojia


Habari kutoka ITV…Mama Maria Nyerere Apongeza Serikali Kwa Kufanikisha Ujenzi wa Daraja la Kigamboni
‘Kwa bahati nzuri nashukuru mwenyezi Mungu amenipa maisha marefu kwasababu hili Daraja lilikuwa lijengwe tangu miaka hiyo ya kwanza na gharama zake walikadiria itakuwa sh. milioni 140 na wakati huo milioni 140 ilikuwa inaonekana ni pesa nyingi sana‘>>>Mama Maria Nyerer


Habari kutoka ITV…Athari za Mvua
Zaidi ya kaya 2000 hazina makazi Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Meck Sadiki ameyaongea haya ‘kuanzia kule juu kote na huku ambapo maji yamepita hakikisheni watu hawa wanahama, sasa niambiwa kuna shamba hapa ambalo limetelekezwa tangu miaka ya 70, nasema viongozi wa vijiji hakikisheni kuwa watu wote waliokuwa kwenye mapito ya maji wanajenga katika mashamba hayo‘>>>Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro


Habari kutoka Star TV...Taa za Kuongozea Magari
Wakazi wa Buzuruga Mwanza Wailalamikia Serikali ‘Kusema kweli hizi taa ni jipu na lina hitaji kutumbuliwa juzi tu tumempoteza mwanamke mwenzetu aligongwa hapa na kupoteza maisha na pia mwanafunzi mwingine aligongwa hapahapa‘>>>Mkazi wa Buzuruga