RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ATOA FAIDA ZA KUSHIRIKI IBADA YA KUFUNGULIWA ILIYOANZA JUMATANO 20 HADI IJUMAA 22/04/2016 NDANI YA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI “B” JIJINI DAR ES SALAAM

Askofu Gertrude Rwakatare naye alikuwa na machache ya kusema katika ibada ya kufunguliwa ya Jumapili 17.04.2016 ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” jijini Dar es Salaam. Alikuwa na haya ya kusema, “ Haleluya Bwana apewe sifa, Je, unaweza kufunga na kuomba kwa siku tatu? 
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare (kushoto) na Mch. Noah Lukumay

 Unajua kufunga kuna maana kubwa sana mbele za MUNGU. BWANA anasema mimi sitawatupa wale wanaojidhiri kwa ajaili yangu, unajua unapofunga unajidhiri, yaani unajinyima kula, kunywa, pale unapoona wenzako ofisini wanakwenda kula wewe unajinyima kwaajili ya MUNGU, unajua huu ni mwezi wetu wa ‘’Deliverance’’ na uzuri tunae Mchungaji wetu Noah Lukumay na tunamuona kabisa kujitoa kwake ajili ya huduma hii ya kufungua watu, mimi nilikuwa naomba tuongeze tena siku za kufunga na kuomba, tufunge tena na kuomba. 
BWANA apewe sifa, hebu tumjaribu MUNGU kwa njia hiyo halafu tuone kama hatafungua madirisha ya Mbinguni na kutubariki, tufunge Jumatano, Alhamisi, na Ijumaa kisha jioni tukutane kwa ajili ya maombi, BWANA apewe sifa halafu MUNGU lazima atafanya njia pale pasipo na njia, MUNGU atafanya mpenyo kwa ajili yako, jamani kilio kiko mahali ukipita mtaani tuseme kama kila nyumba tungeuliza kama ingekuwa ni misiba ya kufiwa basi mahema yangekuwa mengi kiasi ambacho hata magari yangeshindwa kupita, kila nyumba kila kilio chake jamani, kama siyo cha deni basi kuna kilio Fulani,
 kuna mtoto mkorofi kama siyo mtoto basi kuna shughuli fulani ambayo imewabana, watu wamenigwa, na kunigwa huku hakuwezi kufunguka bila kufunga na kuomba. BWANA apewe sifa, Mimi nilikuwa naomba sana jamani kwa sababu sisi tegemeo letu kubwa ni hili, mikono ya watu ni kama imefungwa, wanafanya kazi lakini hela wanazozipata unakuta ni ndogo, mtu anawekeza shilingi milioni tano lakini faida unakuta ni shilingi laki nne tu, 
sasa unafanya nini jamani milioni tano nimewekeza jamani si ni angalau ningepata milioni mbili, lakini unakuta hata milioni tatu hupati, pengine unaishia kutapeliwa hizo roho ni lazima tuzikatae kwa Jina la Yesu, amina. Watu wanapata mishahara lakini mishahara ile kwa kweli unakuta hata haitoshelezi, yaani tunaishi tu kwa neema, yaani kama watu wanaishi tu kwa udanganyifu ni Tanzania, mtu anakwenda nyumbani na mshahara wake ni laki mbili na nusu, hivi kweli laki mbili na nusu na una familia ya watoto wanne, yaani tunaishi tu kwa neema yaani ni neema tu BWANA inatufunika, 

Bwana Yesu apewe sifa, lazima tumsukumize BWANA anapofanya na sisi tufanye na si kumuachia tu Mungu hata kama amekubeba na wewe shughulika, mtie moyo MUNGU. Bwana asifiwe sana tulikua tunatafakari andiko hapa katikati ya wiki ile

Hagai 1;6-9 Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo, mnakula lakini hamshibi, mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji, mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto, nay eye apataye mshahar, apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotobokatoboka.BWANA wa majeshi anasema anasema hivi zitafakarini njia zenu. Pandeni milimani mkalete miti mkaijenge nyumba ya BWANA, 
 nami nitafurahia, name nitatukuzwa asema BWANA. Mlitazamia vingi kumbe vikatokea vichache, tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha, ni kwa sababu gani? Asema BWANA wa majeshi. Ni kwa sababu ya nyumba yangu inayokaa hali ya kuharibika wakati ambapo ninyi mnakimbilia kila mtu nyumbani kwake. 

Mmepanda vingi halafu mme vuna kidogo mtu anayepanda vingi si lazima anavuna vingi lakini unapanda vingi lakini unakuta umevuna kidogo kwanini? BWANA anasema tafakari njia zako mambo yasipo kua mstari katika nyumba, mambo yasipo kwenda sawa katika nyumba yako, hakuna mtu mwingine wa kutafakari ili kuleta mabadiliko katika nyumba yako bali ni wewe. 
Tuwe na siku tatu za kutafakari mbele za BWANA anasema mmekua na tamaa ya kujivika nguo mmejivika lakini bado hamjaridhika, na wanawake ndivyo tulivyo,kila uzi unataka ikitoka ya pinki unataka, ikitoka kitenge unataka, ikitoka chochote unataka, kuvaa hakuna mwisho, tutafakari njia zetu anasema wanao pata mishahara wanaitia kwenye mifuko iliyo toboka toboka hivi wewe utatoboa kusudi hand bag yako kutoka kazini pesa zidondoke mpaka kufika nyumbani huna hela? 
Sasa tuzibe, kila vitobo katika mifuko yetu tuzibe tushone kwa njia ya kufunga na kuomba, kila kizibo kinacho dondosha pesa zangu ovyo ovyo jamani kwanini mimi napoteza hela hivi hivi nilikua na milioni moja naona imeyeyuka, jamani nilikua na milioni mbili imeyeyuka kwa hasara hasara sijanunua hata matofali wala nini, hela inaenda hivi hivi. 
Lazima tukatae hiyo hali jamani sisi ni watawala kila kitu kinachoonekana duniani kipo chini ya miguu yetu, tunayo mamlaka ya kuseta kila aina ya mateso yanayo wapata wa mataifa, sisi si watu wa kawaida. Wewe ni mtoto wa mfalme BWANA apewe sifa ungana pamoja nasi tunapo funga na kuomba kuanzia jumatano,alhamisi na ijumaa jinyime mpaka saa kumi na mbili utakula, BWANA asifiwe sana na sisi tulifunga siku tatu si unatuona hatujafa ndio kwanza tuna ng’aring’ari sura zimekua kama za watoto. Haleluya anasema maana ishara hii haipatikani bali kwa kufunga na kuomba.















Comments