MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE NA JOPO LA WACHUNGAJI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" WAWAPAKA MAFUTA YA UPAKO WAUMINI WA KANISA HILO

Ilikuwa siku ya Jumapili ya 03.04.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ambapo waumini wa kanisa hilo na wasio waumini wa kanisa hilo waliweza kupakwa mafuta ya upako na watumishi wa Mungu wakiongozwa na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Ibada hii ilihohudhuriwa na maelfu ya watu ilifanyika baraka sana kutoka na kile kitendo cha kupakwa mafuta.

Kanisa hili limekuwa na mazoea ya kuwapaka waumini wa kanisa hilo mafuta kwa kipindi fulani ili kufuta na kuondoa nuksi na mikosi inayowakumba katika majumba yao au maofisini mwao. Mafuta haya ya upako yameleta "impact" kubwa sana na baadhi ya waliopakwa mafuta wamekuwa wakishuhudia jinsi Mungu alivyoweza kuingilia kati katika maisha yao.

Mafuta haya ya Upako yanapatikana katika kanisa la Mlima wa Moto, kama ulikuwa na shida yoyote au mgonjwa wako yuko hospitalini, unaweza kufika katika kanisa hili na kuweza kusaidiwa. Kupitia mafuta hii watu wanaona huruma za Mungu zikifanya kazi mahali walipo.

Sasa ni zamu yako ya kupokea baraka hizi na uwe mmojawapo ya watu watakaoshuhudia jinsi  Mungu alivyoweza kufanya kazi katika maisha yako kupitia mafuta haya ya upako yalioombewa na watumishi wa Mungu wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"
 Kulia ni Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
 Mzee wa kanisa (kushoto)
 Katibu wa Kanisa Mzee Kibona akisubiri kupakwa mafuta (aliyepiga magoti)
 Mch. Elizabeth akimpaka mafuta ya upako muumini wa kanisa hili
 Prisca akiwa amepiga magoti tayari ya kupakwa mafuta ya upako
 Mchungaji kutoka Congo akisubiria kupakwa mafuta ya Upako na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
 Mch. Fransis Machichi akigawa mafuta ya upako
0