RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BWANA ANAKUFUNGUA KATIKA MATESO KWASABABU ANA HAJA NA WEWE NA SIO KITU KINGINE.


Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” siku ya Jumapili ya KUFUNGULIWA KWAKO iliyofanyia 17.04.2016 aliweza kufundisha juu ya kujitambua kuwa Mungu anapokufungua katika mateso yako ananakuwa amekusudia wewe kumtumikia na kwahiyo Mungu anakuwa na haja na wewe. Sasa naomba uungane na Bisho kwa kujifunza hili alilohubiri siku hiyo, “Naona ukifunguliwa katika , biashara yako, afya yako. Kila kilichopinda katika maisha yako kimefunguliwa. Wengine afya zao zimepinda mahali hapa, hawaishi maisha ya raha, maisha yao hayaendi bila dawa, hawezi kuondoka nyumbani bila kunywa dawa. Watu wamekuwa na kapresha fulani. Shetani kawatesa kwa miaka mingi, sijui wewe kakutesa kwa miaka mingapi mpaka unasema wewe huwezi kuishi bila dawa, nyumbani kwako ni kama pharmacy una dawa ya asubuhi, ya mchana, na jioni. Mwenyewe umezoea kujipa dawa kwa sababu afya yako ina matatizo. 
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Yesu alipokuwa anahubiri akamuangalia Yule mwanamke akamuhurumia, akamwambia, ‘’Mama kuanzia hivi sasa umefunguliwa.’’ Ugonjwa wake ukamtoka, na mimi leo ninahubiri kuwa siku ya leo ni siku ya BWANA hivyo nasema afya yako imefunguliwa, leo magonjwa ya kisukari yametoka . BWANA apewe sifa, Je unataka kufunguliwa? 

Yesu alikuwa anaenda zake na wanafunzi wake kule Yerusalemu, ndipo akawaambia wanafunzi wake wawili, ‘’Muende mkamfungue Yule mwana punda kisha mwambieni Bwana ana haja naye’’, Sasa wewe haufunguliwi eti kwa sababu wewe upate kufaidi, bali unafunguliwa kwasabau Bwana ana haja na wewe, ni lazima ufunguliwe kwa sababu Bwana ana haja na wewe, Bwana anataka kukutumia, hufunguliwi ili uende uka-enjoy ila Bwana ana haja na wewe, ndio maana anafungua biashara yako kwa sabaubu anajua utatoa fungu la kumi, Bwana anakufungua kwa sababu anajua wewe una huruma unahurumia watu hauli peke yako, kwa hio utafunguliwa kwa sababu Bwana ana haja na wewe, biashara yako inafunguliwa kwa sabau Bwana ana haja na wewe, yale mahusiano ya nyumbani na watoto wako yaache kidogo kwa sababu Bwana ana haja na wewe. Naomba MUNGU akuguse katika maisha yako”. Mungu akubariki sana na usikose ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi.ibada yako tangia nyumbani unaingia kwenye dala dala unanyeshewa na mvua, mungu anakuona.

Comments