MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

DUNIA IMEFIKA MWISHO SASA
Sayari ya Nibiru ikionekana kuikalibia Dunia kwa kasi.


Stori: Oscar Ndauka, UWAZI
DAR ES SALAAM na mitandao: Ile Sayari ya Nibiru au Planet X ambayo wanasayansi duniani wamedai inaielekea dunia kwa kasi ya ajabu na huenda ikaipiga, habari mpya ni kwamba imekaribia lakini pia tukio la kupatwa kwa jua, Septemba Mosi, mwaka huu inazidi kuwapa hofu wanasayansi hao kuwa dunia imefikia ukingoni, Uwazi limechimba.

Kwa mujibu wa taarifa za kisayansi, sayari hiyo iliyogunduliwa mwaka 1982 na Taasisi ya Anga za Juu ya Marekani (Nasa) ikiwa nyuma ya Sayari ya Pluto ambayo ni ya mwisho, inakimbia kwa kasi ya maili 200 kwa sekunde.

MAKADIRIO YA WANASAYANSI
Katika taarifa yao ya hivi karibuni, wanasayansi wa nchi za Ulaya walisema Nibiru ingeipiga dunia Machi 2015, 2016 au 2017 ambapo Mapco sasa wanaendelea na uchunguzi zaidi.

MWELEKEO WAKE
Waliongeza kuwa tangu kuonekana kwake mwaka 1982, sayari hiyo inayowakunisha vichwa wanasayansi duniani, imeshika mwelekeo wa moja kwa moja kuifuata dunia bila kwenda kulia au kushoto hivyo kuwa na wasiwasi kwamba itaigonga dunia na kusababisha mlipuko mkubwa.

IMEANZA KUONEKANA DUNNING
Awali, sayari hiyo ilikuwa ikionekana na vifaa maalum kama vile satelaiti lakini kwa sasa inadaiwa kuwa baadhi ya nchi kama Canada, Marekani hasa maeneo ya Alaska na baadhi ya nchi za Ulaya hususan za Scandnavia zimeanza kuiona sayari hiyo kwa karibu wakati jua linapochomoza asubuhi na kuwa kama ‘majua’ mawili.

HAKUNA KIZAZI KINGINE
Katika kuitafiti sayari hiyo, wanasayansi wamegundua kuwa huingilia mzunguko wa jua (solar system) kila baada ya miaka 3600, jambo linaloonesha wazi kwamba baada ya kutokea safari hii, hakuna kizazi kilicho hai sasa kitakachoshuhudia tena tukio hilo.


Shehe mkuu wa Mkoa wa Dar, Alhadi Mussa Salim.


TUKIO LA AJABU KUONEKANA ANGANI
Tafiti za wataalam hao zinasema kuwa, itakapokuwa kwenye anga la dunia, sayari hiyo itaonekana mfano wa mwezi hivyo wanadamu kuona angani kuna miezi miwili yenye ming’ao sawa, jambo ambalo litashangaza wengi.

DALILI KWAMBA IPO JIRANI NA DUNIA
Matetemeko ya ardhi, vimbunga, milipuko ya volcano na tsunami vinaelezwa kuwa ni dalili ya kwamba sayari hiyo imeingia kwenye mzunguko wa dunia.

KAMA HAITAGONGA DUNIA
Uchambuzi zaidi unasema kuwa kama Nibiru haitavaana na dunia, basi itatumia muda wa wiki 7 au siku kama 51 kupita kwenye anga la dunia na kutokomea zake huku ikisemekana kwamba, wanasayansi wa mashirika makubwa kama Nasa watatangaza kwenye vyombo vya habari itakapofika kabisa ambapo karibu watu wote duniani wataiona.

WACHUNGAJI WAUNGANISHA NA KITABU CHA MUNGU
Baadhi ya watumishi wa Mungu, wameingiza ujio wa Nibiru kuwa umeandikwa katika Biblia, Kitabu cha Ufunuo wa Yohana, Sura ya 8: 10-11, usemao; Malaika wa tatu akapiga baragumu, nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, ilikuwa ikiwaka kama taa. Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga. Theluthi ya maji ikawa pakanga na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalitiwa uchungu.
Malaika wa nne akapiga baragumu, theluthi ya jua ikapigwa na theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota ili kwamba ile theluthi itiwe giza, mchana usiangaze theluthi yake wala usiku vivyohivyo.

MATAMKO YA VIONGOZI WA DINI
Uwazi lilizungumza na viongozi mbalimbali wa dini waliopatikana kwa simu au kwa kutumia maneno ya nyuma kwenye mahubiri yao.POLYCARP KADINALI PENGO.


\ALHADI MUSSA SALIM; yeye ni Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alisema:
“Hizo zote ni dalili kubwa kwa Mungu kututaka wanadamu tujue Mungu yupo maana tumemsahau sana. Hapo hakuna kutishana, watu wamrudie Mungu, adhabu yaja.”
POLYCARP KADINALI PENGO
Yeye ni Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Katika mahubiri yake amekuwa akisisitiza wanadamu kumrudia Mungu kwa vile wakati wa hukumu umekaribia japokuwa haijulikani siku wala saa.

ALEX MALASUSA
Ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Kama alivyo Pengo, sehemu kubwa ya mahubiri yake amekuwa akisisitiza wanadamu kumrudia Mungu kwa kutenda mema wakati wote.

ZACHARY KAKOBE
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel & Bible Fellowship, yeye alisema: “Mwisho wa dunia umekaribia. Hakuna kukwepa wala kupakana mafuta, wanadamu watubu sasa kwa kuwa saa ya hukumu imefika. Hayo yote ni dalili tosha.”

MAMA GETRUDE RWAKATARE
Ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Assemblies of God Mikocheni B ‘Mlima wa Moto’, yeye alisema: “Watu wasali jamani, hukumu ya Mungu inakaribia.”

MAALIM HASSAN
Ni mnajimu na mtabiri mkubwa nchini, yeye anasema: “Kwanza kupatwa kwa jua au mwezi kwa siku hizi ni mara kwa mara tofauti na zamani. Hii ni ishara ya ujio wa maangamizi makubwa duniani.”
KUPATWA KWA JUA, SEPTEMBA MOSI


Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel & Bible Fellowship, Zacharia Kakobe.


Kwa upande wa kupatwa kwa jua, Septemba Mosi, mwaka huu, kulikosemwa na Nasa, wanasayansi wanasema ni kwa ajabu sana kwani nchi zitakazoona tukio hilo, nyingine itakuwa asubuhi ya saa moja, jambo ambalo ni nadra kwani mara nyingi jua hupatwa mchana, alasiri na kuelekea jioni.
Taarifa rasmi zinasema kuwa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ndiyo itakuwa na giza totoro siku hiyo kwa dakika 3 na sekunde 6 za mnato hivyo kuingia kwenye historia ya dunia. Itaanza saa 12:13 na kudumu hadi saa 3:01.
Tayari wanasayansi na watalii kote duniani, wameanza kuwasili jijini Mbeya kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

Mtandao wa Nasa umesema kwamba tukio la kupatwa kwa jua wilayani Mbarali litaonekana asubuhi na wananchi wataweza kulishuhudia kwa kutumia vifaa maalum.
Pamoja na Tanzania, nchi nyingine zitakazoshuhudia tukio hilo litakaloanzia kwenye Bahari ya Atlantic ni Gabon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mauritania, Congo Brazzaville, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Msumbiji na kumalizia Madagascar.

Mapito ya tukio hilo kwenye tovuti ya Nasa yanaonesha kuwa, hapa nchini, litaanza kuonekana Katavi na kupitia Sumbawanga (Rukwa), Mbeya, Songea na Tunduru (Ruvuma), Masasi (Lindi) na kupita Kaskazini ya Msumbiji kisha kumalizikia nchini Madagascar.
0