MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

KANISA JIPYA LA MLIMA WA MOTO GEZAULOLE KIGAMBONI LAPANULIWA

Baada ya watu kuongezeka katika kanisa jipya la Gezaulole Kigamboni, utawala wa kanisa la Mlima wa Moto na mwanzilishi wa makanisa ya Mlima wa Moto duniani Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wakaona ni vyema kuliongeza ukubwa ili watu waweze kukaa kwa nafasi. Kanisa hili lilifunguliwa rasmi miezi miwili iliyopita na sasa limekuwa ni tishio Kigamboni, watu wanaacha uchawi na nguvu za giza wanakimbilia kwa Yesu kwa Yesu. 

Tuzidi kuiombea huduma hii ya Mlima wa Moto ili izidi kusonga mbele na kuwaleta watu kwa Yesu.Kuna watu wanataabika sana na wanakosa msaada, watu hawa wanahitaji kusaidiwa, na kutokana na hilo kanisa la Mlima wa Moto likaona ni vyema kujenga kanisa jipya la Mlima wa MotoKigamboni ambao limeleta "Impact" kubwa sana kwa wakazi wa Kigamboni.

Mbali na kuwa katika ujenzi pia idadi ya watu wanaokoka inazidi kuongezeka kila itwapo Jumapili. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa neema hii aliyoiachia katika kanisa hili la Mlima wa Moto. Kazi ya Bwana inazidi kushamili na watu wanazidi kumrudia huyu Bwana wetu Yesu Kristo. Kama Wakristo tunaomba tushirikiane kuiombea huduma hii isonge mbele na watu wamjue huyu Bwana wetu tumpendae Yesu Kristo. Mch. Stanley Nnko wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" akichapa kazi0