MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MAKONDA ASEMA MWISHO WA OMBAOMBA DAR APRILI 18/2016


Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akitoa taarifa yake kwa wanahabari.

….Akifafanua jambo ambapo kulia kwake akiwa ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro.

Baadhi ya wanahabari wakichukua matukio katika hafla hiyo.

MWENYEKITI wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema mwisho wa ombaomba jijini Dar sasa umefika mwisho kwani kuanzia Aprili ya Jumatatu wiki ijayo kutakuwa na oparesheni kali dhidi yao.

Taarifa hiyo ameitoa leo mchana katika makao makuu ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya oparesheni iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwaondoa ombaomba katika maeneo mbalimbali ya katikati ya jiji.

Makonda amesema hakuna sababu ya ombaomba kuendelea kukaa barabarani na kusababisha usumbufu kwa waendesha magari kuwaomba misaada wakati wengi wao wana sehemu ya kuishi na hasa akisisitiza kwamba asilimia kubwa wana familia zao.
Alifafanua kuwa mji hauwezi kuendelea kuwa na watu wa namna hiyo wanaosababisha usumbufu mkubwa hasa katika sehemu za mataa ya kuongozea magari na kuwataka wenyeviti wa serikali za mitaa kuhakikisha maeneo yao hayana ombaomba yeyote ili kufikia Jumatatu wawe hawapo kabisa katika jiji, na watakaokiuka agizo hilo watakuwa wamepuuza agizo.

“Nirudie tena kuwasisitiza wenyeviti wa serikali za mitaa ambao bado maeneo yao yanakaliwa na madada-poa, makaka-poa wanaofanya biashara za kuuza miili yao kuwachukulia hatua mara moja ili jiji letu liwe chachu ya kivutio na siyo chachu ya kero kwa jamii hivyo. Kwa asiyefuatilia eneo lake sitamvumilia,” alisema Makonda.

NA DENIS MTIMA/GPL
0