RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCH. NOAH LUKUMAY AFUNDISHA JUU YA "MTU WA NNE" ASISITIZA WATU KUBEBANA AU KUSAIDIA WALIO NYUMA YAKO

Mch. Noah Lukumay siku ya Jumapili ya 10.04.2016 katika ibada ya “KUFUNGULIWA” ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” aliweza kufundisha juu “Mtu wa Nne” na alisisitizia watu kubebana, na hivi ndivyo alivyofundisha, 
“Yaani ni kama mtu anayekuvuta nyuma wakati unatakiwa kuwabeba wengine. Utakuta mtu anabeba mzigo wa mtu ambaye hapaswi kubebwa. Watu wanashindwa kubeba mzigo wa kanisa lao wanaenda kubeba mizigo ya makanisa mengine, wanashindwa kuwasaidia watu wa nyumbani mwao wanajikita kuwasaidia wengine. Sio vibaya kusaidiana ila angalia na nyumbani kwako kuna uhitaji gani? .

Ni lazima uchumi wako uungane na yeye anayekulea kiroho, ili kwamba anapomuomba YEHOVA , aweze kukuombea na wewe kwani umekuwa msaada kwa kanisa lako, ili ubarikiwe na kanisa libarikiwe kupitia baraka ulizoombewa na kiongozi wako wa Kiroho.

Sasa hivi tumeitisha siku 3 za “Kufunguliwa Kwako” (Deliverance) - Jumatano, Alhamisi na Ijumaa lakini kuna wengine wataenda kwenye upako mwingine, utajiuliza ni kwanini? Haamini upako wa kanisani kwake, imani yake ni hafifu, halafu bado anajiita mtoto wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”. 
Mtu huyo ambaye hatulii mahali pamoja utaona kanisani kwake ni Mzee wa kanisa wakati huo huo kanisa jingine ni Shemasi. Mtu huyo akitoka hapa anakwenda kuwa Shemasi wa sehemu nyingine ameva badge (kitambulisho cha shingoni) ambacho si cha kanisa lake. 
Mtu huyu haeleweki anatoka wapi anaenda wapi. Wewe unatuchanganya kama umeshaamua njia moja toka nje wapishe wengine, maana Bwana ana watu wake, wewe ukizila wengine wako tayari, wewe ukikataa wengine watafanya, usije ukajidai kwa sababu yoyote BWANA atainua hata mawe. Usije ukasema wewe ndiye unasimamia hii Huduma, ingekuwa imekwishakufa kama ingekuwa ni mwanadamu ndiye anayeisimamia hii Huduma. 
Nachokuomba ni kujitambua wewe ni nani na lipi ni kanisa sahihi kwako kuliko kurukaruka tu na huna msimamo, unachukua ha huku unapeleka kule. Jitambue. Mungu akubariki. Usikose ibada ya Jumapili saa 3 asubuhi.

Comments