MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MCH. NOAH LUKUMAY KATIKA SOMO LAKE LA WATU WANNE ALIFUNDISHA JUU YA KUTOJITENGA NA KUKAA PEKE YAKO KATIKA IBADA YA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Mch. Noah Lukumay siku ya Jumapili 10.04.2016 katika ibada ya Kufunguliwa ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” jijini Dar es Salaam aliweza kufundisha juu ya “Mtu wa Nne” na alisisitiza watu wasiwe wa kujitenga na kukaa peke yao, alisema, “Wapendwa mbona wewe unakaa peke yako? 

Uko na nani kanisani kila mtu anatembea kivyake, akiingia kanisani anakaa peke yake, aliyekuja nyuma yake hamjui ni nani, anavyotoka kanisani baada ya ibada utadhani yuko kweny gwaride akiamurishwa nyuumaa geuka, mbeleee tembea. 

Makanisani kila mtu anafanaya yake bila kusaidiana (wanajitenga) ,wote wanakimbia kama wanafukuzwa, hakuna mtu anayebeba mwenzake. Tunashindwa kwa sababu hatubebani, wewe huwezi ukamuita “Mtu wanne” kwenye matatizo ya ndoa ya mtu wakati wewe huombi naye wala huna mpango naye ila unajifanyia yako. 

Lazima tubebane wapendwa kwenye safari hii yuko shetani anataka kutuangamiza lakini kama tukishikana hata aje kwa mbinu gani ni lazima tutamshinda tu kwa damu ya mwana kondoo na kwa Neno la ushuhuda. Kwa nini mnara wa Babeli uligoma? 

Ni kwa sababu walikuwa wana lugha moja, Je, una lugha ya kanisa la Mlima wa Moto? Ama umebeba Huduma nyingine nyuma? Unahama kanisa lako linaanguka na unasapoti makanisa mengine ambayo hayajakulea wakati unashida. 

Wewe unasupport huduma gani? Moyo wako umebeba huduma gani? Ama umebeba Mitume wengine wadogo wadogo na wakubwa wakubwa wako nyuma yako? Maana yake unaweza ukawa hapa lakini fungu la kumi unatolea kwa T.B Joshua au kwa Ben Hill halafu unasema mama Dr. Gertrude Rwakatare nahitaji uniombee, mama nitembelee, mama nina matatizo. Mama anabeba mzigo wako wakati wewe hauko na yeye unamlemea Mtumishi wa MUNGU.”

0