RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCH. NOAH LUKUMAY: WAZEE WA KANISA TUSITEGEANE KAZI

Mch. Noah Lukumay siku ya Jumapili 10.04.2016 aliweza kufundisha juu ya “Mtu wa Nne” na alisistiza juu ya Wazee wa kanisa kujitoa kufanya kazi ya Mungu, na hivi ndivyo alivyosisitiza, “Je, unahitaji Baraka? Mbona hauji kwenye Chama? Mbona hauji kwenye vijana? Mbona hauji kwenye maombi? Mbona hautaki kukaa na ndugu zako? Wewe unakaaga na nani? 
Unatembeaga na nani? Kwenye kikosi cha maombi hauko, kanisani haueleweki kama ni Mzee wa Kanisa, ama Shemasi au ni nani? Umebaki kuwa na jina tu lakini kazi haionekani unazofanya kanisani kwako. Wewe Mzee ni wa kanisa wa kuja na kutoa sadaka, yaani ukishatoa sadaka tayari umemaliza unaondoka. Siku za katikati ya wiki hauonekani hata hauulizii, ‘’Jamani humo kanisani kuna matatizo gani? Hujui maendeleo ya kanisa. 
Hautaki hata kuomba wenzako wakuonyeshe kitu cha kufanya kanisani kwako, hauonyeshi kuwa kwa wiki una mzigo wa kufanya kazi ya BWANA. Huna muda wa kutambua kuwa kanisani kwako hali ya hewa sio nzuri kwani kuna feni hazifanyi kazi na watu wanapata shida ya joto, unatakiwa sio kununua tu feni na kuondoka bali umsimamie tu na kumwambia fundi feni hii tengeneza, ile tengenezi. Ukiona vyombo vya muziki vinasumbua inabidi ushtuke na kusema, “Eeh hivi naomba mniletee fundi wa vyombo hivi vyombo nasikia vinakoloma koloma.’’ 

Wewe unataka wachungaji waombe feni, waafunge feni, unataka washuhudie au wasimamie mafundi kufunga feni, unataka wafanye nini wapendwa? Unataka wafanye jambo gani na nyie mmekaa? Mchungaji wako au Askofu wako afagie kanisa, adeki choo, afagie uwanja, jamani maji yanamwagika pale nje hakuna mtu anayesema alete kifusi, jamani lori moja ni shilingi ngapi? Wewe unaenda kula “weekend” na watoto wako, lakini kazi ya BWANA imelala, na huku unamuhitaji mtu wa nne ashuuke akusaidi wakati wa shida zako wakati wewe hufanyi kazi ya Mungu bali umekuwa mtu wa kuja kanisani na kutoka. Huna hata muda wa kuangalia maua ya kanisa lako hasa madhabahuni. 
Utaona maua a mapambo yana muda mrefu mpaka yameshika vumbi na wewe upo tu kanisani. Unaweza ukajiuliza hivi huko kwako hakuna maua? Kuna zile zinaiitwa “Palm tree” unazijua, lakini nyumba yako imependeza kuliko hata kanisa lako unaloambudia ili ubarikiwe, umekuwa mnyonyaji unamdhrumu MUNGU wako… duh hii ni hatari sana!!. 

Watu tunasubiri Krismasi au sherehe ndio zitupambie kanisa, madhabahu, jamani ni aibu mbele za watu na mbele za Mungu Hii imekuwa wimbo hakuna mtu anayeweza kudesign, ama ku- plan ya kwamba napaswa kutembea na JEHOVA kupitia hiki ninachotoa na kuchangia muonekano mzuri wa kanisa langu. 

Unaweza uakasema, “Aah…Mch. Noah Lukumay amepanga kutusema….”. Nakuambia sijapanga nakuhakikishia mbele za BWANA, hapa ninachikizungumza sijakiandaa wala sijakiandika. Ni lazima BWANA akiruhusu kije kwako ili upone kwa kutii nachosema au usipone kwa kutotii kwako, ufurahi au usifurahi. Nachotaka kusema ni kwamba sijawekwa hapa ili nikufurahishe, nimewekwa hapa ili nikifika mahali ambapo BWANA ataniuliza kuwa ulikuwa na watu wa Mlima wa Moto umewasaidia kwa njia ipi? Kuna kipindi utaona watu ibadani wanaimba, eti;- 




‘’Gusa gusa gusa moyo wangu BWANA, 
gusa gusa gusa moyo wangu BWANA, 
gusa gusa gusa moyo wangu BWANA 
naamini ukinigusa nitakuwa salama.’’




Atakugusaje na wakati wewe hautaki kumgusa BWANA kwa matoleo yako au kufanya kazi anazokuagiza? Mguse Yeye kwanza. 

Askofu wangu Bishop Dr. Gertrude Rwakatare naona sasa watu hawafurahii hiki ninachowaambia kwasababu kinagusa maisha yao, lakini mimi ninatimiza kile nilichopewa na Mungu niwafikishie ili wapone. Naona sasa watu hawachekelei wala kupiga makofi kama wanavyopigaga ukiwaambia Pooookeeeeaaa Barakaaaa, kwa sababu siwafurahishi, lakini “Niko kwa ajili ya kazi moja siko kwa ajili ya pesa bali ni kwa ajili ya JEHOVA”, Mimi sasa nanawa mikono kwani nimefikisha ujumbe nilioambiwa na Mungu nikuletee Jumapili ya leo. Jamani tumezoea ujumbe wa “mtu wa nne” wa kuruka na kupokea lakini kibao kimegeuka siku ya leo, nashangaa roho ameniammbia waache wairuke lakini waambie ukweli, waache wasifurahie lakini waambie kweli. 
Maandiko yanasema, ‘’Utaifahamu kweli na hiyo kweli itakuweka huru’’

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare unaweza kuona anazeeka lakini siyo kwa sababu umri umeenda hapana ni kwa sababu mzigo unamuelemea, anahiitaji watu wa kubeba majukumu yako, akiwaona watu kati kati ya wiki wanaulizia majukumu moyo wake unafurahi, akisikia kuwa umeingia kwenye utawala unaulizia, ‘’Jamani kuna nini hapa kinachotakiwa kifanyike? Jamani hivi kuna nini huko kanisani? Hebu nipeni ratiba niielewa vizuri’’ fanya kazi yako hujui lini unakufa. 
Hivi MUNGU akakuambia, ‘’Umebakiza siku 50 za kuishi’’ nakuambia utakuwa hautoki hapa, hautoki hapa utasemaMchungaji nabailisha kapeti, Mchungaji nitaleta sijui maji, Mchungaji nahitaji nifanye kitu Fulani, umeambiwa siku 50 tu yaani moyo wote, utakuwa unamwambia MUNGU, ‘’Tengeneza maisha yangu huko, natengeneza maisha yangu huko, ili Yesu akija anikute niko tayari’’
 kumbe unatengeneza siku ukiambiwa umebakiza siku 50, unatafuta yatima wako wapi hapa kanisani, unatafuta ‘’jamani wajane wako wapi ambao hawavai viatu hapa kanisani, nina boksi la viatu limejaa vingine sivivai na vingine vimeshabadilika rangi kwa sababu sivai.’’ Kwanini usilete hapa ukasema jamani hili kabati linanigasi wacha niliiiiivute ili watu wengine wavae na wakivaa ufalme wa JEHOVA utatukuzwa, wewe umebakiza nguo nyumbani viatu unavyo zaidi ya pea 50 wakati hauvai wakati ukifa utavaa pea 1 tu. Kwa Jina la Yesu


Comments