TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MCHINA ALIYEUAWA NDANI YA GARI KIJITONYAMA HUYU HAPA


Polisi wakichukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi.

Mfanyabiashara raia wa China aliyetambulika kwa jina la Luo Dongpeng (32), maiti yake imekutwa ndani ya gari lenye namba za usajili T145 DFY Machi 28, mwaka huu maeneo ya Kijitonyama, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar, Uwazi linakupasha.
Gari aina ya Nissan X-Trial alimokutwa amenyongwa mchina huyo.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo wanaoishi maeneo aliyokutwa Mchina huyo zinaeleza kuwa, gari la marehemu huyo walianza kuliona hapo tangu alfajiri ya siku hiyo. Na watu wengine waliweza kupita mida ya saa 10 alfajiri waliliona hilo gari wakajua ni gari la wenye nyumba. 

Ilipofika mchana mtoto mmoja wa eneo hilo akiwa anacheza nje ya eneo hilo aliamua kusogelea katika gari hilo na kuangalia ndani kuna nini maana ni muda mrefu gari analiona, alipochungulia ndipo aliona mtu ameegama kwenye kiti cha nyuma ya dereva akiwa na damu. Mtoto huyo aliamua kwenda kuita wazazi wake na walipoangalia kwa makini waliona mtu amefariki ndipo wazazi hao waliwaita majirani  ili washuhudie tukio hilo.

Waliendelea kusema kwamba ilipofika saa 10.00 jioni walilazimika kulisogelea na kuchungulia ndani ndipo walipomuona mtu akiwa amelala kiti cha nyuma, walipomwamsha hakuamka wala kujigeuza ndipo waliwaarifu polisi wa Kituo cha Mabatini Kijitonyama.

Moja ya msumali uliokuwa umetegwa kwenye gari hilo.

Mashuhuda hao walidai kuwa huenda Mchini huyo aliuawa kisha kutelekezwa na gari lake maeneo hayo kwani alikuwa na michubuko mikononi na shingoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Alphonce Fuime alipohojiwa na gazeti hili wiki iliyopita ofisini kwake alikiri kutokea kwa mauaji hayo.

Mashuhuda wakiwa kwenye tukio hilo.

“Huyu marehemu inaonekana alikuwa akitoka casino na uchunguzi wa awali unaonesha aliuawa sehemu nyingine na akutupwa hapo.Tunaendelea na uchunguzi kuwasaka watu aliokuwa nao casino kwa mara ya mwisho,” alisema Kamanda Fuime aliyefafanua kuwa mwili huo ulipelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
0