RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCHUNGAJI: JPM AANDALIWE MKESHA WA MAOMBI


Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’

Stori: Oscar Ndauka, WIKIENDA
DAR ES SALAAM: Neema ya Mungu! Mchungaji wa Kanisa la AGCT, Mbagala, Samuel Mihogu amewataka watumishi wengine wa Mungu nchini hususan wa jijini Dar kufanya mpango kwa kuchagua siku moja ili kukesha kwa maombi ya kumlilia Mungu azidi kumlinda Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’, Wikienda lina maneno yake.

Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar, Mchungaji Mihogu alisema kuwa, kwa mwendo wa Magufuli kikazi anaamini atazalisha maadui, hivyo watumishi wa Mungu wanatakiwa kumwomba Mungu ashushe ulinzi wake juu ya rais ili wabaya wake washindwe kwa kuanzia.

“Magufuli anafanya kazi kubwa sana na nzito. Kutetea kwake wanyonge kwa kuwatumbua vigogo wanaokula pesa za umma lazima kuna watu hawatapenda, kwa hiyo mimi nawaomba wachungaji wengine tupange namna ya kutafuta siku moja tu ya kukesha Uwanja wa Taifa au Leaders (Dar) kwa maombi ili kumlilia Mungu amshushie ulinzi.

“Najua serikali inampa ulinzi wa kutosha lakini maandiko yanasema mlinzi wa kweli ni Mungu. Kwa hiyo pamoja na ulinzi wa serikali, lakini Mungu lazima ahusike,” alisema mchungaji huyo.

Akaendelea: “Kuhusu kulindwa hata Magufuli mwenyewe analijua ndiyo maana katika hotuba zake zote anawaomba Watanzania wamwombee kwa vile kazi anayoifanya ni ngumu

Comments