MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MH. PAUL MAKONDA APONGEZWA NA WASANII WA BONGO MOVIE KUWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM

Mh. Paul Makonda mwenye hofu ya Mungu na mnyenyekevu mbele za watu ameweza kupongzwa na  mastaa mbalimbali wakiwemo wa Bongo Movies wakijisevia msosi wakati wa hafla hiyo.WASANII wanaounda Kundi la Bongo Movie wakiongozwa na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ usiku wa kuamkia leo wamefanya sherehe fupi ya kumpongeza Mhe. Paul Makonda aliyeapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Shughuli hiyo iliyohudhuriwa na mastaa mbalimbali wa filamu ilifanyika kwenye hoteli ya Rodizio iliyopo maeneo ya Masaki jijini Dar, ambapo miongoni mwa wasanii waliokuwepo ni Steve, Jacob Steven ‘Jb’, Aunt Ezekiel, Blandina Chagula ‘Johari’ na wengineo.
Kwa upande wake, Mhe. Paul aliwashukuru wasanii hao kwa kutambua mchango wake na kumuandalia hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisalimiana na msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel.
Mboni Masimba akimpatia Paul Makonda zawadi ya keki.
Steve Nyerere akitoa neno katika hafla hiyo.
RC Paul Makonda akiongea na mastaa mbalimbali wa Bongo katika hafla hiyo ya kumpongeza.


Mwanamuziki Mrisho Mpoto naye akitoa nasaha zake kwa Mhe. Paul Makonda.
Blogger William Malecela ‘Lemutuz’ naye akichangia mada wakati wa hafla hiyo.
Steven Jacob ‘JB’ akiongoza sala ya ufunguzi wa hafla ya kumpongeza Mhe. Paul Makonda.


Paul Makonda akichukua chakula katika hafla hiyo ya kumpongeza.

Picha / Habari: Musa Mateja na Mayasa Mariwata/ GPL
0