RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MIGOGORO SUGU YA KWAYA NA DAWA YA KUZIFANYA ZISIFE - MWALIMU JOHN MTANGOO - See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/#sthash.rv7ovycU.dpuf



Moja ya kwaya maarufu duniani ya Soweto Gospel Choir wakiwa jukwaani

MIGOGORO SUGU YA KWAYA
Kwaya nyingi kama sio zote zinafanana tabia. Tofauti ya ukubwa wa migogoro inatokana na ukomavu wa kwaya. Mgogoro ambao kwaya hii itaupuuza kwa kwaya ingine unatosha kuipeleka kaburini.

1. MIGOGORO YA FEDHA
Kwaya nyingi hazina mfumo mzuri wa kutunza fedha. Viongozi wa juu wamekuwa sio waaminifu. Nikipokea kwaya inayotaka kurekodi changamoto kubwa ni kuongeza bei kuliko makubaliano halisi. Kuna kwaya nilirekodi Audio & Video kwa 3,200,000/= lakini nilikuja kuona gharama iliyoandikwa ni 7,000,000/=. Mauzo ya CD kwaya nyingi hazijui mapato na matumizi. Michango inayopokelewa haiendi kwenye matumizi yaliyoainishwa. HII IMEVUNJA MOYO WAIMBAJI WENGI NA WAKAAMUA KUACHA KUIMBA KWAYA.

2. MAJUNGU NA FITINA
Kama kuna kiti cha enzi cha shetani kwenye kwaya ni hapa. Kuna wakati unajiuliza hivi waimbaji wakiacha kusengenyana na kuzuliana mambo watakosa nini? Ikitokea mtu anasolo HASA KWA WANAWAKE ujue atasemwa mpaka akose hamu ya kuimba. Waimbaji wanashindwa kuendeleza vipaji vyao kwa kuogopa maneno. Hii dhambi ni ya kukemewa hasa!

3. UZINZI.
Sikuwa nimejua kwa nini Babu yangu CANON ELISHA MTANGOO alikuwa akisisitiza sana juu ya waimbaji kuoana wao kwa wao. Kumbe kukiwa na wanandoa ndani ya kundi kunafanya walindane juu ya uzinzi. Wadada wengi kwenye kwaya hawaolewi sababu wamechezewa sana. Wakaka wengi hawaoi kwenye kwaya maana wanajua jinsi wamewapiga danadana wadada wao. Nilishawahi kuamua ugomvi wa mwenyekiti na mwalimu wanamgombania solo. WADADA JIFUNZENI KUSEMA NO MUHESHIMIKE!

-TUFANYE NINI KWAYA ZISIFE?-
1. Msingi wa uimbaji ni mwimbaji kujua kusudi la Mungu ndani yaje kumchagua kutumika.
- Kwaya sio kijiwe cha wasio na kazi
- Kwaya sio sehemu ya kupitishia muda.
- Kwaya ni mamlaka kamili ya sifa kutoka kiti cha enzi cha Mungu.

2. Maombi ndiyo injini inayoendesha kusudi la Mungu. Waimbaji wengi hukimbia vipindi vya maombi. Wakimaliza kuhudumu hawapendi kukaa na kujifunza neno la Mungu. Ukitaka zoezi likose watu tangaza kutakuwa na maombi au neno. KWAYA NYINGI ZINAKUFA KWA KUKOSA MAARIFA AMBAYO NI NENO LA MUNGU.

3.Uongozi lazima uwe na ubunifu wa matukio. Recording ya Audio na video. Safari za karibu na mbali. Mikesha, matamasha mradi vivutio visipungue. Kwaya inakaaje mwaka mzima haijasafiri? Unakaaje hata hujaenda basi kanisa jirani?

4. MUONEKANO. Kwaya yenye muonekano wa kiutu uzima inakubalika sana kwa wafadhili. Kwaya yenye vijana inavutia vijana wengi kujiunga. KUMBE MCHANGANYIKO WA UMRI UNAONGEZA UHAI WA KWAYA. Ni vema kufanya uinjilisti unaopelekea kwaya kuwa na mchanganyiko wa makabila. Mfano wachaga hawana vipaji lakini ni wazuri wa mipango lakini wagogo wana vipaji lakini ni waoga!

5. Kuwa na wanamuziki wengi na walimu wengi.
- mtunzi wa nyimbo asiwe mmoja. Akiwa peke yake lazima atawasumbua tu!
- mziki ni ulimbo. Wanamuziki wanatabia ya kuvutana. Jiandae kupata wanamuziki wageni kama idara yako ya mziki itakaa sawa.

6. Kwaya ijifunze kujitegemea. Ubunifu wa miradi ni muhimu sana. Kuna miradi inafungua ajira kwa waimbaji.

7. Ukiona muimbaji au mwanamziki mzuri yuko mahali na ana ujuzi fulani, tumia nafasi hiyo kumshawishi ili ujuzi huo alionao, umtafutie ajira kwa manufaa ya kwaya.
Mungu anamakusudi kwa kila kuanzishwa kwa kundi. Kiongozi wa kundi andika maono ya kundi, yaweke kwenye maombi yaambatanishe na sadaka Mungu atakusimamishia kundi.
BARIKIWA. 

John Mtangoo 2016.Mtayarishaji Na Mwalimu Wa Muziki Wa Gospel Tanzania

Comments